• HABARI MPYA

  Wednesday, June 01, 2016

  MBEYA CITY WAFUATA MAKALI YA MSIMU MPYA MALAWI

  TIMU ya Mbeya City inatarajiwa kufanya ziara ya michezo ya kirafiki nchinin Malawi katikati ya mwezi huu.
  Mbeya City  imepaga kucheza michezo mitatu Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre kuanzia Juni 18  dhidi ya vigogo wa soka nchini humo, Big Bullets, wakati Juni 21 itamenyana na Civo United.
  Mechi nyingine Mbeya City wataijua baada ya kufika nchini humo na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri anataka kuitumia ziara hiyo kuanza maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kikosi cha Mbeya City msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAFUATA MAKALI YA MSIMU MPYA MALAWI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top