• HABARI MPYA

  Sunday, December 13, 2015

  YANGA SC YAMTEMA KIPA ‘CHA UVIVU’, ASAINI JKT MGAMBO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imemtema kipa Mudathir Khamis iliyemsaini mwanzoni mwa msimu kutoka KMKM ya Zanzibar.
  Na mara moja, kipa huyo amesaini timu nyingine ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mgambo JKT ya Tanga.
  Yanga SC ilimpa Mkataba mnono wa miaka mitatu, Mudathir na mshahara wa Sh. Milioni 1.3 kwa mwezi, lakini baada ya miezi mitano inamtema.
  Katibu wa Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha amesema kwamba wamelazimika kumuacha kipa huyo baada ya kushindwa kuonyesha bidii na kuwashawishi makocha.
  Mudathir Khamis ametemwa Yanga SC baada ya miezi mitano akidaka mechi moja tu ya kirafiki

  “Ni pendekezo la benchi la ufundi, walisema hawawezi kuendelea na huyo mchezaji, kwa sababu haonyeshi bidii kabisa mazoezini na kwa ujumla amekuwa mvivu,”amesema Tiboroha.
  Aidha, Katibu huyo amesema kwamba alitaka kumtoa kwa mkopo kumpa nafasi ya kubadilika, lakini hakuna timu hiyo ilitokuwa tayari kumchukua, ndipo wakaamua kuachana naye.
  Lakini imekuwa bahati nzuri kwake, Mudathir amesaini JKT Mgmabo.
  Tangu ametua Jangwani, Mudathir amedaka mechi moja tu ya kirafiki dhidi ya Kemondo kirafiki, Yanga SC ikishinda 4-1. Yanga inabaki na makipa watatu, Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benedicto Tinocco.
  Mudathir alisani miaka mitatu Yanga SC Agosti mwaka huu na kupewa mshahara wa Milioni 1.3 kwa mwezi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMTEMA KIPA ‘CHA UVIVU’, ASAINI JKT MGAMBO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top