• HABARI MPYA

  Sunday, December 13, 2015

  LIVERPOOL CHUPUCHUPU KWA WBA, WATOA SARE 2-2, NEWCASTLE YANG’ARA UGENINI

  MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND
  Leo; Desemba 13, 2015  
  Liverpool 2 - 2 West Bromwich 
  Tottenham Hotspur 1 - 2 Newcastle United
  Aston Villa 0 - 2 Arsenal
  Jana; Desemba 12, 2015  
  Bournemouth 2 - 1 Manchester United
  Crystal Palace 1 - 0 Southampton
  Sunderland 0 - 1 Watford
  Manchester City 2 - 1 Swansea City
  West Ham United 0 - 0 Stoke City
  Norwich City 1 - 1 Everton

  Mshambuliaji wa Liverpool, Divock Origi akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha ikitoa sare ya 2-2 na Weat Bromwich PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  BAO la Divock Origi dakika ya 96 limeinusuru Liverpool kulala mbele ya West Bromwich Albion, baada ya kutoa sare ya 2-2 usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
  Jordan Henderson alianza kuifungia Liverpool dakika ya 21, kabla ya Craig Dawson kuisawazishia West Bromwich Albion dakika ya 30 na Jonas Olsson kufunga la pili dakika ya 73.
  Mchezo mwingine wa usiku huu, Newcastle United wamepata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane.
  Eric Dier alianza kuifungia Spurs dakika ya 39, kabla ya Aleksandar Mitrovic kuisawazishia Newcastle United dakika ya 74 na Ayoze Perez Gutierrez kufunga la pili dakika ya 93.
  Awali ya hapo, Arsenal ilirejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 jioni ya leo dhidi ya wenyeji Aston Villa Uwanja wa Villa Park.
  Ayoze Perez akiifungia Newcastle bao la ushindi baada ya kutokea benchi leo Uwanja wa White Hart Lane PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Ushindi huo, umeifanya The Gunners ifikishe pointi 33 baada ya kucheza mechi 16, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 32, sawa na Leicester City wakati Manchester United sasa ni ya nne kwa pointi zake 29.
  Mabao ya Arsenal leo yamefungwa na Olivier Giroud kwa penalti ya utata dakika ya nane baada ya The Walcott kuonekana ameangushwa na lingine Aaron Ramsey dakika ya 38.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL CHUPUCHUPU KWA WBA, WATOA SARE 2-2, NEWCASTLE YANG’ARA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top