• HABARI MPYA

  Sunday, December 13, 2015

  JKT RUVU YAITANDIKA 4-1 PRISONS LIGI KUU, AFRICAN SPORTS YATOKA SARE NA COASTAL

  MATOKEO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo; Desemba 13, 2015
  JKT Ruvu 4 - 1 Prisons
  Coastal Union 1 - 1 African Sports
  Jana; Desemba 12, 2015
  Mgambo JKT 0 - 0 Yanga SC
  Kagera Sugar 1 - 1 Ndanda FC
  Stand United 0 - 2 Mwadui FC
  Mbeya City 2 - 2 Mtibwa Sugar
  Azam FC 2 - 2 Simba SC
  Majimaji 1 - 5 Toto Africans
  Samuel Kamuntu ameifungia JKT leo
  JKT Ruvu imezinduka baada ya kuitandika Prisons mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya JKT Ruvu inayofundishwa na kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ ifikishe pointi nane baada ya kucheza mechi 11 na kuanza kujiondoa kwenye hatari ya kuteremka daraja.
  Mabao ya JKT Ruvu leo yamefungwa na Michael Aidan mawili, Samuel Kamuntu na Mussa Mussa, wakati la kufutia machozi la Prisons limefungwa na Mohammed Mkopi.
  Mchezo mwingine wa ligi hiyo leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ‘mahasimu’ wa jiji hilo, African Sports na Coastal Union wametoshana nguvu baada ya kutoka sare ya 1-1.
  Mechi za jana, Mgambo JKT ilitoka 0-0 na Yanga SC, Kagera Sugar ilitoka 1-1 na Ndanda FC, Mwadui FC iliifunga 2-0 Stand United, Mbeya City ilitoka 2-2 na Mtibwa Sugar, Azam FC ilitoka 2-2 na Simba SC na Toto Africans iliichapa 5-1 Majimaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT RUVU YAITANDIKA 4-1 PRISONS LIGI KUU, AFRICAN SPORTS YATOKA SARE NA COASTAL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top