• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2015

  SAMATTA AINGIA FAINALI TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA, WAMEBAKI WATATU TU

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameingia tatu bora ya Tuzo ya Mwanasoka Bora Nayecheza Afrika.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika iliyotumwa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE mchana huu imesema Samatta ameingia fainali na kipa Robert Kidiaba anayecheza naye TP Mazembe ya DRC na Baghdad Boundjah wa Algeria na Etoile du Sahel ya Tunisa.
  Katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Jumla wa Afrika, walioingia fainali ni Andre Ayew wa Ghana na Swansea City, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund na Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester City, anayeshikilia tuzo hiyo.
  Kila la heri Mbwana Ally Samatta, ameingia fainali tuzo za Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika

  Majina hayo yametangazwa mchana wa leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Abuja, Nigeria na washindi wapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na makocha wakuu wa timu za taifa au Wakurugenzi wa Ufundi wa Vyama na mashirikisho ya soka ya nchi zote wanachama wa CAF.
  Washindi watatangazwa katika usiku wa tuzo za Glo-CAF Januari 7 mwaka 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AINGIA FAINALI TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA, WAMEBAKI WATATU TU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top