• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2015

  ETOILE DU SAHEL YAINGIA TUZO YA KLABU BORA YA MWAKA AFRIKA

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya vipengele vingine vya tuzo zake za mwaka 2015, maarufu kama Tuzo za Glo-CAF. 
  Vipengele hivyo ni Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka, Mchezaji Chipukizi wa Mwaka, Mchezaji Anayechipukia Mwenye Kipaji, Kocha wa Mwaka, Refa wa Mwaka, Gwiji wa Afrika, Timu ya Taifa ya Mwaka, Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka, Klabu ya Mwaka na na Tuzo Maalum ya Platinum.
  Orodha hiyo imetangazwa leo mjini Abuja, Nigeria katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliohudhuriwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Anjorin Moucharafou na wawakilishi wa Glo, ambao ni wadhamini.
  Washindi watapatikana baada ya kura zitakazopigwa kupitia CAF Footbal kasoro tu kwa tuzo ya Gwiji na Platinum, wakati ya Referee wa Mwaka itaamuliwa na kura za Kamati ya Marefa ya CAF.
  Washindi watataangazwa katika usiku wa tuzo za Glo-CAF Alhamisi ya Januari 7, mwakani mjini Abuja, Nigeria.
  Etoile du Sahel imeshindanishwa na TP Mazembe, USM Alger na Orlando Pirates tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka Afrika 

  Mchezaji wa Kike wa Mwaka
  ·         Gabrielle Onguene, Cameroon
  ·         Gaelle Enganamouit, Cameroon
  ·         Ngozi Ebere, Nigeria
  ·         N'rehy Tia Ines, Ivory Coast
  ·         Portia Boakye, Ghana
  Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka  
  ·         Adama Traore, Mali
  ·         Kelechi Nwakali, Nigeria
  ·         Samuel Diarra, Mali
  ·         Victor Osimhen, Nigeria
  ·         Yaw Yeboah, Ghana
  Chipukizi Mwenye Kipaji Zaidi       
  ·         Azubuike Okechukwu, Nigeria
  ·         Etebo Oghenekaro, Nigeria
  ·         Djigui Diarra, Mali
  ·         Mahmoud Abdelmonem ‘Kahraba’, Misri
  ·         Zinedine Ferhat, Algeria
  Kocha wa Mwaka 
  ·         Baye Ba, Mali, U17
  ·         Emmanuel Amunike, Nigeria U17
  ·         Fawzi Benzarti, Etoile Sportive de Sahel
  ·         Hervé Renard, Ivory Coast
  ·         Patrice Carteron, TP Mazembe
  Refa wa Mwaka
  ·         Alioum, Cameroon
  ·         Bakary Papa GASSAMA, Gambia
  ·         Eric Arnaud OTOGO CASTANE, Gabon
  ·         Ghead Zaglol GRISHA, Misri
  ·         Janny SIKAZWE, Zambia
  Gwiji wa Afrika
  ·         Charles Kumi Gyamfi, Ghana
  ·         Samuel Mbappe Leppe, Cameroon
  Timu ya Taifa ya Mwaka
  ·         Ivory Coast
  ·         Ghana
  ·         Mali U17
  ·         Nigeria U17
  ·         Nigeria  U-23
  Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka
  ·         Ghana
  ·         Cameroon
  ·         Afrika Kusini
  ·         Zimbabwe
  Klabu ya Mwaka
  ·         USM Algers , Algeria
  ·         TP Mazembe, DRC
  ·         Orlando Pirates, Afrika Kusini
  ·         Etoile Sportive du Sahel, Tunisia
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ETOILE DU SAHEL YAINGIA TUZO YA KLABU BORA YA MWAKA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top