• HABARI MPYA

    Monday, December 14, 2015

    PAUL NONGA ATUA YANGA SC, WINGA WA NIGER APEWA MWAKA MMOJA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC ya Shinyanga, Paul Nonga anatarajiwa kusaini Yanga SC.
    Nonga aliyejiunga na timu ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ msimu huu kutoka Mbeya City, ametumiwa tiketi ya ndege awahi haraka Dar es Salaam kusaini kwa ‘Vimwaga Fedha’ hao katika usajili, Yanga SC.
    BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE inafahamu mshambuliaji huyo amependekezwa na kocha Msaidizi, Juma Mwambusi ambaye alifanya naye kazi Mbeya City miaka miwili iliyopita.
    Pamoja na Nonga, Yanga SC ipo mbioni kumsajili winga wa Niger, Issoufou Boubacar Garba baada ya majaribio ya siku mbili mjini Tanga.
    Paul Nonga (kulia) anatarajiwa kusaini Yanga SC akitokea Mwadui FC

    Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amempendekeza mchezaji huyo wa zamani wa 
    Club Africain na ES Hammam-Sousse za Tunisia asajiliwe baada ya kumjaribu kwa siku mbili mfululizo katika mazoezi mjini Tanga.
    Garba aliyezaliwa mji wa Niamey, mwenye urefu wa futi 5 na inchi 6, kisoka alianzia klabu ya AS FAN ya kwao mwaka 2010, kabla ya kuhamia Thailand ambako alichezea klabu za Muangthong United mwaka 2011 na Phuket.
    Mwaka 2012 alitua Club Africain ya Tunisia ambako hakucheza mechi hadi anahamishiwa 
    ES Hammam-Sousse ambako pia hakucheza.
    Wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka ES Hammam-Sousse hajapata timu nyingine, lakini uongozi wa Yanga SC umejiridhisha anachezea klabu bingwa ya kwao, AS Douanes.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAUL NONGA ATUA YANGA SC, WINGA WA NIGER APEWA MWAKA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top