• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2015

  OKECHUKWU AWA MCHEZAJI BORA MICHUANO YA U-23 AFRIKA

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemtaja Nahodha wa Under-23 ya Nigeria, Azubuike Okechukwu (pichani juu) kuwa Mchezaji Bora wa mashindano ya U-23 Afrika yaliyomalizika mwishoni mwa wiki nchini Senegal.
  Kiungo huyo wa Yeni Malatyaspor ya Uturuki amepewa ushindi huo na Kikundi cha Tathmini za Kiufundi cha CAF (TSG) baada ya mashindano.
  Okechukwu alitoa mchango mkubwa Nigeria kutwaa ubingwa wa Afrika wa U-23, wakiifunga Algeria katika fainali mabao 2-1.
  Kinda huyo wa umri wa miaka 18 amecheza mechi zote kasoro moja ya Nusu Fainali, kutokana na kuwa anatumikia adhabu za kadi ambayo Nigeria iliwatoa wenyeji, Senegal.
  Mshambuliaji wa Warri Wolves, Oghenekaro Etebo ameibuka mfungaji bora wa mashindano kwa mabao yake matano, wakati kipa wa Algeria, Abdelkadir Salhi amekuwa mlinda mlango bora wa michuano.
  Afrika Kusini imeshinda tuzo ya timu yenye Nidhamu, wakati Nigeria limekuwa taifa lililofunga mabao mengi katika mashindano, baada ya kupata jumla ya mabao tisa katika mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKECHUKWU AWA MCHEZAJI BORA MICHUANO YA U-23 AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top