• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2015

  MAN UNITED YAPEWA WADENMARK 32 BORA EUROPA LEAGUE, LIVERPOOL NA WAJERUMANI

  Manchester United itamenyana na Midtjylland katika hatua ya 32 ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  RATIBA YA EUROPA LEAGUE HATUA YA 32 BORA 

  Valencia vs Rapid Vienna 
  Fiorentina vs Tottenham
  Borussia Dortmund vs  Porto
  Fenerbache vs Lokomotiv Moscow 
  Anderlecht vs Olympiacos 
  Midtjylland vs Manchester United
  Augsburg vs Liverpool 
  Galatasaray vs Lazio
  Sparta Prague vs FC Krasnodar 
  Sion vs Braga 
  Shakhtar Donetsk vs Schalke
  Marseille vs Athletic Bilbao 
  Sevilla vs Molde
  Sporting vs Bayer Leverkusen
  Villarreal vs Napoli
  St Etienne vs Basle 
  (Mechi za kwanza zitachezwa Alhamisi ya Februari 18 na marudiano yatakuwa Alhamisi ya Februari 25, mwaka 2016) 
  TIMU ya Manchester United imepangwa na timu dhaifu, Midtjylland ya Denmark katika hatua ya 32 Bora ya Europa League.
  Baada ya kutolewa na Wolfsburg katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, kikosi cha Louis van Gaal sasa kimeangukia Europa League.
  Midtjylland ambayo ilianzishwa tu mwaka 1999 baada ya muungano wa klabu mbili, walitwaa taji lao la kwanza la ligi msimu uliopita.
  Liverpool, ambayo kocha wake, Jurgen Klopp anahofia kukutana na timu yake ya zamani, Dortmund, itamenyana na timu nyingine ya Ujerumani, Augsburg.
  Augsburg iliwashangaza wengi baada ya kumaliza juu ya Dortmund na Schalke katika Bundesliga msimu uliopita.
  Tottenham ndiyo imekutana na shughuli pevu, baada ya kupewa have Fiorentina ndani ya mwaka mmoja baada ya kutolewa na timu hiyo ya Serie A kwenye mashindano hayo.
  Valencia ya Hispania ya kocha Muingereza, Gary Neville imepangwa na Rapid Vienna na mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa Februari 14 wakati marudiano yatakuwa wiki inayofuata.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAPEWA WADENMARK 32 BORA EUROPA LEAGUE, LIVERPOOL NA WAJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top