• HABARI MPYA

    Tuesday, September 01, 2015

    MWAIKIMBA AWAADHIBU AZAM FC, WAPIGWA 2-1 NA JKT RUVU CHAMAZI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Gaudence Mwaikimba (pichani) usiku huu ameiadhibu timu yake ya zamani, Azam FC akitoa mchango mkubwa kwa timu yake mpya, JKT Ruvu kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo, ambao kocha Muingereza Stewart Hall aliwakosa nyota wake wa kikosi cha kwanza walio na timu za taifa, JKT Ruvu walipata bao la kwanza dakika ya 10 Mwaikimba akimalizia shuti la Mussa Said akitumia makosa ya kipa Mwadini Ali.
    Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha kupitia kwa Kipre Herman Tchetche dakika tano baadaye, akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya JKT.
    JKT Ruvu inayofundishwa na beki wa zamani wa Yanga SC, Freddy Felix Minziro ilipata bao lake la ushindi dakika ya 85 mfungaji Najim Magulu aliyemalizia pasi ya Mwaikimba baada ya beki Bryson Raphael kuchanganyana na kipa wake Mwadini Ali.
    Mchezo huo ulikuwa maalum kwa timu zote kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza wiki ijayo.
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Serge Pascal Wawa, Gardiel Michael, Lacine Diouf/Said Mourad dk47, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Bryson Raphael, Ame Ally, Kipre Tchetche na Ramadhani Singano ‘Messi’/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk60. 
    JKT Ruvu: Tony Kavishe, Napho Zubery, Edward Charles, Cecil Kisimba, Martine Kavila, Hamisi Shengo, Ismail Mohammed/Emanuel Pius dk20, Matheo Daniel/Issa Ngao dk80, Gaudence Mwaikimba, Amour Janja/Najim Magulu dk76 na Mussa Said/Jaffar Kisoky dk80.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWAIKIMBA AWAADHIBU AZAM FC, WAPIGWA 2-1 NA JKT RUVU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top