• HABARI MPYA

    Friday, September 25, 2015

    PLUIJM ANAJUA SIMBA SC IMEMPA ULAJI MARA MBILI YANGA SC, LAKINI...

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MAKOCHA wawili wamefukuzwa Yanga SC ndani ya miaka miwili kwa sababu ya Simba SC. Hao ni Mholanzi Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts na Mbrazil Marcio Maximo Barcellos.
    Pamoja na kuipa Yanga SC ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2012-2013, lakini Brandts alitupiwa virago baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba SC Desemba 23 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Mabao ya Simba SC siku hiyo yalifungwa na Amisi Tambwe mawili dakika ya 14 na 44 kwa penalti na Awadh Juma, wakati bao pekee la Yanga lilifungwa Emmanuel Okwi dakika ya 87.
    Yanga SC wakaachana na Brands na kumuajiri Mholanzi mwenzake, Hans van der Pluijm ambaye mwishoni mwa msimu wa 2013-2014 alishindwa kubakiza taji la ubingwa wa Ligi Kuu Jangwani, likichukuliwa na Azam FC.
    Pluijm akaondoka pamoja na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa kwenda kufundisha Al Shoalah FC ya Saudi Arabia na Yanga SC ikamuajiri Mbrazil Maximo, ambaye baada ya miezi mitano akafukuzwa kufuatia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Simba SC Desemba 13, mwaka jana katika mchezo wa Nani Mtani Jembe 2, mabao ya Awadh Juma na Elias Maguri. 
    Hans van der Pluijm akarudishwa Jangwani Januari mwaka huu, akimalizia vizuri msimu kuwa kuiwezesha Yanga SC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, lakini naye akafungwa na Simba SC katika mechi ya Ligi Kuu Machi 8, mwaka huu, bao pekee la Okwi dakika ya 52.
    Kwa ujumla, Pluijm hakuwahi kuifunga Simba SC hata kabla ya kwenda Uarabuni, kwani alipokutana nayo awali Aprili 19, mwaka jana katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu msimu wa 2013- 2014 alitoa nayo sare ya 1-1, bao la Wekundu wa Msimbazi likifungwa na Haroun Chanongo dakika ya 76 na Yanga akifunga Simon Msuva dakika ya 86.
    Pluijm anajua fika aliletwa Yanga SC mara ya kwanza baada ya kufukuzwa Mholanzi mwenzake, Brandts kufuatia kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba. Na anajua fika alirudishwa Yanga SC kufuatia kufukuzwa kwa Maximo baada ya kipigo cha 2-0 cha Simba SC.
    Na anajua hajawahi kuifunga Simba SC. Na anakumbuka alifungwa na Simba SC iliyoonekana ‘kibonde’ Machi mwaka huu. Yote hayo yapo kichwani mwake kuelekea mchezo wa kesho Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Katika kipindi chake cha awali, Pluijm aliiongoza Yanga SC katika mechi 19, akishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, moja tu nyumbani 2-1 mbele ya Mgambo JKT mjini Tanga, nyingine akifungwa na Al Ahly 1-0 katika Ligi ya Mabingwa Afrika mjini Alexandria Misri. 
    Na aliporejea Januari mwaka huu, hadi sasa ameiongoza Yanga SC katika mechi 44 za mashindano yote, akishinda 29, sare saba na kufungwa nane. Kwa ujumla Pluijm ameiongoza Yanga SC katika mechi 63, akishinda 40, sare 13 na kufungwa 10. 
    Hans van der Pluijm (kushoto) anajua mara mbili zote ameajiriwa Yanga SC baada ya kufukuzwa kwa makocha waliofungwa na Simba SC

    REKODI YA PLUIJM YANGA SC
                  P W L D
    JUMLA: 63 40 10 13
    MARA YA KWANZA
    Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki)
    Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki)
    Yanga SC 2-1 Ashanti United (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
    Yanga SC 5-2 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
    Yanga SC 7-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu ya Bara)
    Yanga SC 1-0 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa)
    Yanga SC 0-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa. Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)
    Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar  (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)
    (Mechi 19, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili)
    Benchi la Ufundi la sasa la Yanga SC; kutoka kulia Daktari Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa na Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm. Kesho watafurahi mbele ya Simba SC?

    ALIVYOREJEA:
    Yanga SC 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 4-0 Polisi (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 1-0 Shaba (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 0-1 JKU (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 0-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-0 Polisi Moro (Ligi Kuu)
    Yanga SC 0-0 Ndanda FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 BDF XI (Yanga SC 1-2 BDF (Kombe la Shirikisho nyumbani)
    Yanga SC 3-0 Priosns (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-2 BDF (Kombe la Shirikisho ugenini)
    Yanga SC 0-1 Simba SC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-1 Platinum FC (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Yanga SC 0-1 FC Platinum (Kombe la Shirikisho Zvashavane)
    Yanga SC 8-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-1 Etoile du Sahel (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 3-2 Stand United (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    Yanga SC 4-1 Polisi Moro
    Yanga SC 0-1 Etoile du Sahel (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 1-2 Azam FC (LIgi Kuu)
    Yanga SC 0-1 Ndanda FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-2 Friends Rangers (Kirafiki Karume)
    Yanga SC 0-0 SC  Villa (Kirafiki Taifa)
    Yanga SC 1-0 KMKM (KIrafiki Taifa)
    Yanga SC 3-0 Polisi Kombaini (KIrafiki Taifa)
    Yanga SC 1-2 Gor Mahia (Kagame Taifa)
    Yanga SC 3-0 Telecom (Kagame Taifa)
    Yanga SC 1-0 Khartoum N (Kagame Taifa)
    Yanga SC 0-0 Azam FC pen (3-5 Robo Fainali Kagame Dar)
    Yanga SC 4-1 Kemondo FC (Kirafiki Mbozi. Mbeya)
    Yanga SC 2-0 Prisons (Kirafiki Mbeya)
    Yanga SC 3-2 Mbeya City (Kirafiki Mbeya)
    Yanga SC 0-0 Azam FC (8-7 penalti Ngao ya Jamii)
    Yanga SC 2-0 Coastal Union (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 3-0 Prisons (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 4-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu Taifa) 
    Maximo alifungwa Yanga SC baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Simba SC Desemba 13, mwaka jana
    (Mechi 44 za mashindano yote, ameshinda 29, sare saba na kufungwa nane).
    Ernie Brandts alifukuzwa na benchi lake zima baada ya Yanga SC kufungwa 3-1 na Simba SC Desemba 23, mwaka juzi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLUIJM ANAJUA SIMBA SC IMEMPA ULAJI MARA MBILI YANGA SC, LAKINI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top