• HABARI MPYA

    Monday, September 21, 2015

    SOMOE 'ANYIMWA' OFISI TWFA LICHA YA USHINDI WA KISHINDO

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    LICHA ya kushinda kwa kishindo nafasi ya Ukatibu Msaidizi wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA), Mwandishi wa mwandamizi wa habari za michezo nchini, Somoe Ng'itu (pichani) bado hajakabidiwa ofisi kwa sababu ambazo hazieleweki.
    Somoe ndiye pia ndiye Kaimu Katibu Mkuu wa TWFA baada ya kushinda Ukatibu Msaidizi mwezi uliofanyika Agosti 29, ndiye anapaswa kuwa Mtendaji wa shughuli za kila siku za chama.
    "Sijui chochote ndugu yangu, kwa sababu bado sijakabidhiwa ofisi, nashindwa kusema chochote,"alisema Somoe leo baada ya kuulizwa kuhusu timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars iliyoshiriki Michezo ya Afrika (AAG) mwezi huu mjini Brazaville, Kongo.
    Twiga imetolewa mapema tu katika hatua ya makundi baada ya kuambulia sare moa na wenyeji Kongo Brazaville na kufungwa na Ivory Coast na Nigeria na tayari imerejea nchini. 
    "Nimejaribu kuwasiliana na Mwenyekiti mara kadhaa, lakini bahati mbaya ametingwa mno, kwa hivyo namsubiri atakapokuwa tayari nitaanza kazi,"aliongeza Somoe baada ya kuulizwa amefanya jitihada gani za kuhakikisha anakabidhiwa ofisi aanze kazi.
    Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa TWFA, Amina Karuma kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa kutokana na kutopatikana katika simu yake mara zote alipotafutwa.
    Somoe, anyeandikia gazeti la Nipashe, alipata kura 34 dhidi ya 18 za mpinzani wake Dk Cecilia Makafu katika uchaguzi mdogo wa TWFA kuwania nafasi ya Katibu Msaidizi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
    Katika uchaguzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa TWFA, Amina Karuma, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho, nafasi iliyoachwa wazi na Linna Kessy, baada ya kupata kura 51 za ndiyo dhidi ya 1 ya hapana kati ya kura 52 zilizopigwa.
    Kufuatia kujiuluzu kwa Karuma katika NAFASI ya ukatibu Mkuu, Wajumbe wa mkutano huo wakairidhia Somoe akaimu nafasi hiyo, hadi pale  mkuu utakapofanyika.
    Wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo mdogo,ni Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji, Debora Mkemwa aliyepata kura 47 na Theresia Mung'ong'o aliyepata kura 45, huku Mwanaheri Kalolo akishindwa baada ya kuambulia kura 11.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SOMOE 'ANYIMWA' OFISI TWFA LICHA YA USHINDI WA KISHINDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top