• HABARI MPYA

    Sunday, September 27, 2015

    AZAM FC ‘YAISULUBU’ MBEYA CITY CHAMAZI, KIPRE TCHETCHE, MUDATHIR ‘OYEE OYEE’

    RATIBA NATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
    Leo; Septemba 27, 2015
    Azam Fc 2-1 Mbeya City
    African Sports 1-0 Ndanda FC
    Jana; Septemba 26, 2015
    Simba SC 0-2 Yanga SC
    Coastal Union 0-0 Mwadui FC
    Prisons FC 1-0 Mgambo JKT
    JKT Ruvu 0-1 Stand United
    Mtibwa Sugar 1-0 Majimaji FC
    Kagera Sugar 0-0 Toto Africans
    Wafungaji wa mabao ya Azam FC, Mudathir Yahya na Kipre Tchetche kushoto wakishangilia na wenzao

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    AZAM FC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa mabao 2-1 Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Saanya wa Morogoro, aliyesaidiwa na Julius Kasitu wa Shinyanga na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, hadi mapumziko Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
    Bao hilo limefungwa na kiungo Mudathir Yahya Abbas dakika ya 10 baada ya kuuwahi mpira uliookolewa kufuatia yeye mwenyewe kupiga shuti la la kwanza, baada ya kupokea pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy.
    Timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza ma Mbeya City walipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 44 baada ya shuti la Joseph Mahundi kugonga mwamba na kurudi uwanjani na kumkuta Serge Wawa Pascal aliyeokoa.
    Kipindi cha pili, mchezo uliendelea kuwa wa staili ile ile, timu zote kushambuliana kwa zamu.
    Kipa wa Mbeya City, Mganda Hannington Kalyesebula akidaka mpira huku beki wake, Juma Nyosso akiwa tayari kumsaidia. Chini ni Nahodha wa Azam Fc, John Bocco  
    Nahodha wa Mbeya City, Juma Nyosso akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche
    Kiungo wa Mbeya City, Steven Mazanda akigombea mpira na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco



    Mshambuliaji Kipre Herman Tchetche kutoka Ivory Coast aliifungia Azam FC bao la pili dakika ya 52 akimalizia pasi ya Sure Boy tena.
    Mbeya City walicharuka zaidi baada ya bao hilo na kuongeza kasi na nguvu ya mashambulizi langoni mwa Azam FC, hatimaye kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Raphael Alpha dakika ya 56.
    Kipre Tchetche aliifungia Azam FC bao ambalo lingekuwa la tatu, lakini refa Saanya akasema mfungaji aliotea.
    Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 12, sawa na Mtibwa Sugar na Yanga SC, zikifuatiwa na Simba SC yenye pointi tisa.
    Mchezo mwingine wa ligi hiyo uliofanyika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga African Sports imepata ushindi wa kwanza, baada ya kuilaza bao 1-0 Ndanda FC.
    Kikosi  cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, David Mwantika, Racine Diouf, Serge Wawa Pascal, Jean Baptiste Mugiraneza, Mudathir Yahya/Himid Mao dk46, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco, Kipre Tchetche/Alan Wanga dk78 na Farid Mussa. 
    Mbeya City; Hannington Kalyesebula, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Juma Nyosso, Christian Sembuli, Steven Mazanda, Richard Peter, Raphael Alpha, George Mlawa/David Kambole dk85, Themi Felix/Meshack Samuel dk58 na Joseph Mahundi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC ‘YAISULUBU’ MBEYA CITY CHAMAZI, KIPRE TCHETCHE, MUDATHIR ‘OYEE OYEE’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top