• HABARI MPYA

    Tuesday, September 22, 2015

    NGASSA AENDELEA KUNG’ARA AFRIKA KUSINI, APIKA MABAO YOTE, FREE STATE YASHINDA 3-2

    Mrisho Ngassa (kulia) akiwa na Mtanzania mwenzake, Uhuru Suleiman aliyekwenda kupiga naye picha baada ya mechi
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa alikuwa kivutio kikubwa leo wakati Free State Stars inaibuka na ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Maritzburg United katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
    Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Harry Gwala, Ngassa alikuwa mpishi wa mabao yote matatu ya FS akicheza nafasi ya kiungo mchezeshaji.
    Bao la kwanza lililofungwa na Danny Venter dakika ya 62 ilikuwa pasi ya Mrisho pamoja na la tatu lililofungwa na na Robert Sankara dakika ya 90.
    Lakini Ngassa aliinua mashabiki Uwanja mzima wa Gwala baada ya kupiga chenga wachezaji wanne wa Meritsburg na alipofika kwenye boksi ili afunge mwenyewe, akaangushwa na kuwa penalti ambayo ilikwamishwa kimiani na Andrea Fileccia  dakika ya 80. 
    Mabao ya Meritburg yalifungwa na Kurt Lentjies kwa penalti dakika ya 65 na Mohammed Anas dakika ya 89. Mchezaji mwingine wa Tanzania, Uhuru Suleiman anayechezea Royal Eagles ya Daraja la Kwanza alikuwepo Uwanja wa Gwala kumtazama mwenzake akipiga kazi Ligi Kuu na baada ya mechi wakapiga picha ya pamoja.
    Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa FS chini ya kocha mpya, Mjerumani Ernest Middendorp aliyerithi mikoba ya Mmalawi Kinnah Phiri aliyejiuzulu mwezi uliopita.
    Mechi yake ya kwanza Middendorp aliiongoza State kushinda 3-0 dhidi ya Chippa United, Ngassa akitoa pasi za mabao ya Andrea Fileccia dakika ya 34 na 84, huku akishiriki shambulizi la bao la Danny Venter dakika ya 77.
    Phiri aling’atuka FS baada ya timu kupoteza mechi tatu mfululizo za mwanzo katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini 1-0 kutoka kwa Mpumalanga Blac Aces, 4-0 kutoka kwa Kazier Chiefs na 2-1 mbele ya Ajax Cape Town.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA AENDELEA KUNG’ARA AFRIKA KUSINI, APIKA MABAO YOTE, FREE STATE YASHINDA 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top