• HABARI MPYA

    Monday, September 28, 2015

    ETOILE WAICHAPA 5-1 ZAMALEK NUSU FAINALI AFRKA, HILAL YALALA 2-1

    MATOKEO NA RATIBA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
    Septemba 27, 2015  
    Al Hilal (Sudan) 2-1 USM Alger (Algeria)
    Septemba 26, 2015  
    Al Merreikh (Sudan) 2-1 TP Mazembe (DRC)
    MECHI ZIJAZO
    Oktoba 3, 2015
    USM Alger (Algeria) Vs Al Hilal (Sudan)
    Oktoba 4, 2015
    TP Mazembe (DRC) Vs El Merreikh (Sudan)
    MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA SHIRIKISHO
    Septemba 27, 2015  
    ES Sahel (Tunisia)  5-1 Zamalek (Misri)
    Septemba 26, 2015  
    Orlando Pirates 1-0 Al Ahly (Misri)
    MECHI ZIJAZO
    Oktoba 3, 2015
    Zamalek (Misri) Vs ES Sahel (Tunisia)
    Oktoba 4, 2015
    Al Ahly (Misri) Vs Orlando Pirates

    Etoile iliitoa kwa shida Yanga SC katika hatua ya 16 Bora 

    TIMU ya Etoile du Sahel ya Tunisia imebisha hodi kwa kishindo Fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka 2015, baada ya kuitandika mabao 5-1 Zamalek ya Misri usiku wa Jumapili mjini Sousse, Tunisia.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Olimpiki, Marouane Tej alifunga mabao mawili dakika za tano na 83 na Baghdad Bounedjah dakika ya 11, Alaya Brigui dakika ya 35 na Saddam Ben Aziza dakika ya 87 wakafunga moja kila mmoja kwa washindi hao wa pili wa LIgi ya Tunisia 2015.
    Zamalek iliyofungwa mabao matatu tu katika mechi zake za awali za ugenini na kuitandika 4-1 Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wake uliopita, ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa Ayman Hefni dakika ya 25.
    Nusu Fainali nyingine ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Jumamosi, Al Ahly walifungwa 1-0 na Orlando Pirates mjini Soweto, bao pekee la Thamsanqa Gabuza.
    Zamalek wataikaribisha Etoile Jumamosi ijayo mjini Cairo na Ahly watakuwa wenyeji wa Pirates Jumapili ijayo mjini Suez.
    Ikumbukwe, Etoile iliitoa Yanga SC ya Tanzania katika hatua ya 16 Bora kwa jumla ya mabao 2-1, ikitoa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kushinda 1-0 Sousse.

    LIGI YA MABINBGWA…
    USM Alger ya Algeria imepata ushindi wa ugenini wa mabao 2-1 dhidi ya El Hilal Jumapili katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa El-Hilal mjini Omdurman.
    Wenyeji ndiyo walioanza kupata bao kupitia kwa Mudather El Tahir dakika ya pili kabla ya USM kutokea nyumba na kushinda kwa mabao ya Mohamed Amine Aoudia dakika ya 13 na 
    Karim Baiteche dakika ya 67.
    Katika Nusu Fainali nyingine ya kwanza jana, El Merreikh ilishinda 2-1 dhidi ya TP Mazembe Uwanja wa Marreikh mjini Khartoum, Sudan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ETOILE WAICHAPA 5-1 ZAMALEK NUSU FAINALI AFRKA, HILAL YALALA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top