• HABARI MPYA

    Tuesday, September 01, 2015

    CHELSEA YASAJILI BEKI LA READING, NI MJAMAICA MICHAEL HECTOR

    KLABU ya Chelsea imefanya usajili wa kushitukiza baada ya kumsaini kwa Pauni Milioni 4.5 beki wa kati wa Reading, Michael Hector ikiizidi kete Crystal Palace.
    Palace ilikuwa inamtaka mwanasoka huyo wa kimataifa wa Jamaica na leo asubuhi ilipeleka ofa, lakini imezidiwa kete na mabingwa wa Ligi Kuu ya England waliofanikiwa kuinasa saini ya kinda huyo wa miaka 23 baada ya Mkurugenzi wa Ufundi wa Chelsea, Michael Emenalo kuvutiwa na mchezaji huyo wiki za karibuni.
    Chelsea imemrudisha kwa mkopo Hector kuendelea kucheza Uwanja wa Madejski hadi mwishoni mwa msimu.
    Michael Hector akiwa na jezi ya Chelsea baada ya kukamilisha ingawa amerudishwa Reading kucheza kwa mkopo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YASAJILI BEKI LA READING, NI MJAMAICA MICHAEL HECTOR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top