• HABARI MPYA

    Tuesday, September 01, 2015

    MAN UNITED YAMSAJILI ANTHONY MARTIAL MIAKA MINNE KWA PAUNI MILIONI 36

    KINDA wa umri wa miaka 19, Anthony Martial amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 36 kujiunga na Manchester United kutoka Monaco katika dili ambalo dau linaweza kupanda hadi Pauni Milioni 58.
    Mchezaji huyo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Ufaransa amesaini Mkataba wa miaka minne katika siku ya leo ya mwisho ya usajili.
    Aliwasili mjini Manchester jana kwa vipimo vya afya  kabla ya kusaini Mkataba leo na kukabidhiwa jezi namba tisa Manchester United, huku Mkataba wake ukiwa na kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja.
    Manchester United imemtangaza rasmi Anthony Martial kutoka Monaco aliyesaini Mkataba wa miaka minne PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAMSAJILI ANTHONY MARTIAL MIAKA MINNE KWA PAUNI MILIONI 36 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top