• HABARI MPYA

    Sunday, July 26, 2020

    YANGA SC YAICHAPA LIPULI FC 1-0 SAMORA NA KUMALIZA KATIKA NAFASI YA PILI LIGI KUU TZ BARA7

    Na Mwandishi Wetu, IRINGA
    VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli FC jioni ya leo Uwanja wa Samora mjini Iringa.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji David Molinga Ndama ‘Falcao’ dakika ya 38 na kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 72, ikizidiwa pointi 16 na mabingwa, Simba SC na wakiwazidi pointi mbili Azam FC waliomaliza nafasi ya tatu. 
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Nassor Mwinchui wa Pwani aliyesaidiwa na Charles Simon wa Dodoma na Anold Bugado wa Tanga, Molinga aliyesajiliwa Agosti mwaka jana kutoka kwao, Kongo alifunga bao hilo akimalizia pasi ya mkongwe, Mrisho Khalfan Ngassa kutoka upande wa kulia.


    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Simba SC imeshinda 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Mabao ya Simba SC yamefungwa yote leo yamefungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco dakika ya pili na 45 na ushei, wakati la Polisi limefungwa na Marcel Kaheza dakika ya 30.
    Tanzania Prisons imelazimishwa sare ya 2-2 na Azam FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Mabao ya Prisons yamefungwa na Abdallah Kheri aliyejifunga dakika ya 11 na Vedastus Mwihambi dakika ya 39, wakati ya Azam FC yamefungwa na Jumanne Elifadhili aliyejifunga dakika ya kwanza na Never Tigere dakika ya 59.
    Mbao FC ikaibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda SC mabao yake yakifungwa na Jordan John dakika ya 66 na Waziri Junior dakika ya 18 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
    Nayo Mtibwa Sugar ikaichapa 2-1 Ruvu Shooting mabao yake yakifungwa na Boban Zilintusa dakika ya 51 na 65 la wageni likifungwa na Saadat Mohamed dakika ya 35.
    Alliance FC ikaibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Mabao ya Alliance FC yamefungwa na Martin Kiggi dakika ya kwanza, Israel Patrick dakika ya 25 na Juma Nyangi dakika ya 65, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Bigirimana Blaise dakika ya nane na Frank Mkumbo dakika ya 61.
    Mbeya City wakaibuka na ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya KMC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam mabao ya Rehani Kibingu dakika ya 68, Abasarim Chidiebele dakika ya 87 na Peter Mapunda dakika ya 90 na ushei kwa penalti.
    Bao pekee la Najim Magulu dakika ya 79 likawapa JKT Tanzania ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Mwadui FC wakaichapa Kagera Sugar 2-1 Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga. Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Wallace Kiango dakika ya 13 na 17 kwa penalti wakati la Kagera Sugar limefungwa na Nasoro Kapama dakika ya 68.
    Biashara United ikaichapa 2-0 Singida United Uwanja wa Liti mjini Singida, mabao ya Deogratius dakika ya 20 na David Nartey aliyejifunga dakika ya 27.
    Kikosi cha Lipuli FC kiliuwa; Isihaka Joseph, David Kameta, Paul Ngalema, David Mwasa, Peter Mwangosi, Fred Tangaro, Shaaban Ada/Ally Liungo dk67, Pius Enos/Seif karihe dk67, Daruwesh Saliboko/Joseph Ntamack dk78, Engbert Kisatya/Rashid Hassan dk57 na Kenneth Masumbuko/Paulo Materaz dk57.
    Yanga SC; Farouk Shikhalo, Juma Abdul, Adeyoum Ahmed, Ally Mtoni ‘Sonso’, Said Juma ‘Makapu’, Abdulaziz Makame, Feisal Salum/ Tarik Seif dk87, Mrisho Ngassa/ Paul Godfrey dk87, Ditram Nchimbi, David Molinga na Yikpe Gislain/Adam Kiondo dk60.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA LIPULI FC 1-0 SAMORA NA KUMALIZA KATIKA NAFASI YA PILI LIGI KUU TZ BARA7 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top