• HABARI MPYA

    Friday, July 10, 2020

    MAN U NA COPENHAGEN AU BASAKSEHIR ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

    TIMU ya Manchester United itamenyana na ama Copenhagen au Istanbul Basaksehir katika Robo Fainali ya UEFA Europa League ikiwa wataitoa LASK.
    Man United pia inaweza kukutana na Wolves katika Robo Fainali itakayohusisha tmu za England tupu.
    Wolves, wao wana mchezo mgumu wa Robo Fainali dhidi ya ama Sevilla au Roma ikiwa wataitoa Olympiacos kwenye hatua ya 16 Bora.

    Manchester United itamenyana na Copenhagen au Istanbul Basaksehir katika Robo Fainali ya  Europa League 


    RATIBA KAMILI EUROPA LEAGUE

    Robo-Fainali:
    Wolfsburg / Shakhtar Donetsk vs Frankfurt / FC Basel 
    Manchester United / LASK vs Istanbul Basaksehir / FC Copenhagen  
    Inter Milan / Getafe vs Bayer Leverkusen / Rangers
    Olympiacos / Wolves vs Sevilla / Roma
    Semi-finals:
    Mshindi RF 4 vs Mshindi RF 2
    Mshindi RF 3 vs Mshindi RF 1 
    Rangers watakutana na Inter Milan au Getafe kwenye Robo Fainali kama watapindua kipigo cha 3-1 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Bayer Leverkusen.
    Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kimetanguliza mguu mmoja Robo Fainali baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya LASK ya Austria kwenye mchezo wa kwanza mwezi Machi.
    Mechi yao ya Robo Fainali dhidi ya ama Istanbul Basaksehir ya Uturuki au Copenhagen ya Denmark itachezwa Agosti Ujerumani. Basaksehir inaongoza 1-0 baada ya mechi ya kwanza.
    Wakati huo huo, Wolves walitoa sare ya 1-1 na Olympiacos ya Ugiriki mwezi Machi, lakini watakuwa na Robo Fainali ngumu dhidi ya Sevilla au Roma, ambao bado hawajacheza mechi hata moja kutokana na kusimama kwa mashindano hayo kwa sababu ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN U NA COPENHAGEN AU BASAKSEHIR ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top