• HABARI MPYA

    Sunday, July 26, 2020

    KAPTENI BOCCO APIGA ZOTE MBILI SIMBA SC YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 UWANJA WA USHIRIKA

    Na Mwandishi Wetu, MOSHI
    MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wamemaliza kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi katika mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Saanya wa Morogoro aliyesaidiwa na Makame Mdogo na Joseph Pombe wa Shinyanga, mabao ya Simba SC yamefungwa yote leo yamefungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco dakika ya pili na 45 na ushei, wakati la Polisi limefungwa na Marcel Kaheza dakika ya 30.
    Kwa matokeo hayo, Simba SC iliyobeba taji la Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu na mara ya 21 jumla, inamaliza na pointi 88, ikifuatiwa na watani wao wa jadi, Yanga SC waliomaliza na pointi 72, wakati Azam FC imemaliza na pointi 70 nafasi ya tatu.


    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Yanga SC wameshinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli FC bao pekee la David Molinga dakika ya 38 Uwanja wa Samora mjini Iringa.
    Tanzania Prisons imelazimishwa sare ya 2-2 na Azam FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Mabao ya Prisons yamefungwa na Abdallah Kheri aliyejifunga dakika ya 11 na Vedastus Mwihambi dakika ya 39, wakati ya Azam FC yamefungwa na Jumanne Elifadhili aliyejifunga dakika ya kwanza na Never Tigere dakika ya 59.
    Mbao FC ikaibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda SC mabao yake yakifungwa na Jordan John dakika ya 66 na Waziri Junior dakika ya 18 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
    Nayo Mtibwa Sugar ikaichapa 2-1 Ruvu Shooting mabao yake yakifungwa na Boban Zilintusa dakika ya 51 na 65 la wageni likifungwa na Saadat Mohamed dakika ya 35.
    Alliance FC ikaibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Mabao ya Alliance FC yamefungwa na Martin Kiggi dakika ya kwanza, Israel Patrick dakika ya 25 na Juma Nyangi dakika ya 65, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Bigirimana Blaise dakika ya nane na Frank Mkumbo dakika ya 61.
    Mbeya City wakaibuka na ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya KMC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam mabao ya Rehani Kibingu dakika ya 68, Abasarim Chidiebele dakika ya 87 na Peter Mapunda dakika ya 90 na ushei kwa penalti.
    Bao pekee la Najim Magulu dakika ya 79 likawapa JKT Tanzania ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Mwadui FC wakaichapa Kagera Sugar 2-1 Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga. Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Wallace Kiango dakika ya 13 na 17 kwa penalti wakati la Kagera Sugar limefungwa na Nasoro Kapama dakika ya 68.
    Biashara United ikaichapa 2-0 Singida United Uwanja wa Liti mjini Singida, mabao ya Deogratius dakika ya 20 na David Nartey aliyejifunga dakika ya 27.
    Kikosi cha Polisi Tanzania kilikuwa; Mohammed Yussuf, William Lucian ‘Gallas’/Shaaban Stambuli dk67, Yassin Mustafa, Mohamed Kassim, Iddi Mobby, Pato Ngonyani, Sixtus Sabilo, Hassan Maulid, Matheo Anthony/Andrew Chamungu dk89, Marcel Kaheza/Jimmy Shoji dk57 na Pius Buswita/Mohamed Mkopi dk57.
    Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Yussuf Mlipili, Kennedy Juma, Gerson Fraga, Luis Miquissone/Deo Kanda dk82, Said Ndemla, John Bocco/Meddie Kagere dk67, Clatous Chama na Francis Kahata/Hassan Dilunga dk82.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAPTENI BOCCO APIGA ZOTE MBILI SIMBA SC YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 UWANJA WA USHIRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top