• HABARI MPYA

  Saturday, December 15, 2018

  MTIBWA SUGAR WAONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA MICHUANO YA AFRIKA, WASHINDILIWA 3-0 NA KCCA LEO KAMPALA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imechapwa mabao 3-0 na wenyeji KCCA katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Philip Omondi mjini Kampala jioni ya leo.
  Mabao ya KCCA, timu inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Kampala leo yamefungwa na Allan Kyambade dakika ya 48, Patrick Kaddu dakika ya 73 na Allan Okelo dakika ya 85.
  Mtibwa Sugar inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Zuberi Katwila ilizidiwa kabisa na KCCA kwenye mchezo wa leo. 

  Wachezaji wa Mtibwa Sugar na KCCA katika mchezo wa leo mjini Kampala

  Kipigo hicho kinaiweka mguu nje Mtibwa Sugar kwenye michuano hiyo, sasa ikihitaji kushinda 4-0 kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo Uwanja wa Azam Complex mjini Dar es Salaam wiki ijayo ili kusonga mbele. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA MICHUANO YA AFRIKA, WASHINDILIWA 3-0 NA KCCA LEO KAMPALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top