• HABARI MPYA

  Wednesday, November 07, 2018

  RAMADHANI SHAURI ASAINI MKATABA WA KUZIPIGA NA AZIZI ULIZA MKESHA WA MWAKA MPYA UWANJA WA KINESI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABONDIA Ramadhani Shauri na Aziz Uliza wame saini mkataba wa kuzipiga Desemba 31, mwaka huu katika Uwanja wa Kinesi uliopo maeneo ya Shekilango mjini Dar es Salaam.
  Akizungumza mratibu wa mpambano uho Chaurembo Palasa amesema kuwa wamejizatiti kuinuwa mabondi yeye na kampuni ya Ijuka Sports ambao wanajishughulisha na kuinuwa mchezo wa masumbwi nchini
  "Mabondia wengi wana ndoto ya kufika Marekani kucheza mchezo wa ngumi, sasa kampuni hii imeanza na mapambano haya ili mradi mabondia wapate nafasi ya kupigana Marekani ambapo mchezo huu unakubalika kwa asilimia mia moja bila kupingwa mabondia,"amesema Mratibu wa pambano hilo, Chaurembo Palasa.

  Mabondia Ramadhani Shauri (kulia) na Aziz Uliza (kushoto) wakitambulishwa na promota Chaurembo Palasa leo

  Aliendelea kwa kusema siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka wakati Hussein Itaba atazipiga na Kanda Kabongo na Tonny Rashidi atazipiga na Nassoro Madimba kutoka Bagamoyo maeneo ya Kiwangwa na Rolen Japhert atazikunja na Mohamedi Kashinde 'Simba wa Mbagala' nae Baina Mazola ataoneshana umwamba na Faraji Sayuni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAMADHANI SHAURI ASAINI MKATABA WA KUZIPIGA NA AZIZI ULIZA MKESHA WA MWAKA MPYA UWANJA WA KINESI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top