• HABARI MPYA

  Thursday, November 08, 2018

  HUMUD ASEMA ANA MKE MZURI KULIKO WACHEZAJI WOTE NCHI HII HAWEZI KUTONGOZA WAKE WA WACHEZAJI WENZAKE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Abdulhalim Humud 'Gaucho' amesema kwamba ana mke mzuri kuliko wachezaji wa Tanzania hivyo, asingeweza kuwatongoza wake wa wachezaji wezake klabu ya KMC.
  Humud amefukuzwa na klabu ya KMC kwa tuhuma za kuwatongoza wake na wapenzi wa wachezaji wenzake wa klabu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.
  Akijibu shutuma hizo, Humud amesema kwamba yeye mwenyewe ana familia ana mke na watoto hivyo hawezi kumvunjia heshima mke wake kwa kutongoza wake wa wachezaji wenzake.   Abdulhalim Humud 'Gaucho' amekanusha tuhuma za kutongoza wake wa wachezaji wenzake

  Alisema kuwa kwanza yeye anamke mzuri sana kuliko wachezaji wote wa Tanzania, maana mke wake akisimama na wake wa wachezaji wezake hawawezi kumfikia, hivyo hawezi kuwa na tamaa ya kutaka wanawake wengine.
  "Siwezi kumdhalilisha mke wangu kwani ni mzuri zaidi kuliko wake zao, hivyo inabidi kuheshimiana na si kuharibiana maisha kwa vigezo vya kusema kwamba ninawatongozea wake zao," amesema Humud.
  Mchezaji huyo wa zamani wa Simba na Azam FC, amesema kwamba anasikitshwa na uongozi wa klabu hiyo kumchafulia jina lake hasa kwa kipindi hiki cha dirisha dogo linalokaribia kufunguliwa.
  Humudi amesema kamwe hajawahi kufanya kitendo hicho kwa wachezaji wezake  bali viongozi hao waameamua kumchafulia.
  Humud alisema kwanza muda mwingi huwa anakuwa kambini na mara nyingi wanafanya mazoezi na kuingia kwenye mechi kwa maana hiyo anakosa muda hata wa kuonana na hao wanawake kutokana na kazi ngumu ya mpira anayofanya.
  "Mimi ni mchezaji mwenye mchezaji mzuri, kwahiyo ikitokea kashfa kama hiyo huwa inaniharibia mimi sababu hiki ni kipinidi cha usajili wa dirisha dogo kunichafua kwa staili hiyo ni kutaka kuniharibia  nisweze kupata nafasi kwenye timu  nyingine.
  Naamini Mungu yupo kutokana na uwezo na juhudi nilizozitumia kuhakikisha KMC inapanda daraja na kuweza kuitumia kwa kipindi chote naamini pia nitaweza kupata timu nyingine ili niweze kuitumikia kwa kipindi hiki cha Ligi Kuu Tanzania bara.
  Hapo awali Humud aliwahi kuzitumikia Simba, Coastal Union na Azam FC, alijiunga na KMC mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HUMUD ASEMA ANA MKE MZURI KULIKO WACHEZAJI WOTE NCHI HII HAWEZI KUTONGOZA WAKE WA WACHEZAJI WENZAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top