• HABARI MPYA

  Wednesday, November 07, 2018

  HIMID MAO ACHEZA MWANZO MWISHO PETROJET YAPIGWA 3-2 UGENINI, ILIONGOZA 2-0 HADI MAPUNZIKO

  Na Mwandishi Wetu, CAIRO
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami jana alicheza kwa dakika zote 90, timu yake, Petrojet FC ikichapwa 3-2 na Nogoom katika mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Petrosport, Al-Qahirah mjini Cairo.
  Kwa matokeo hayo, Petrojet inaendelea kushika nafasi ya 17 katika Ligi ya timu 18 ikiwa imevuna pinti 10 katika mechi 12 ilizocheza, wakati Haras El Hodood yenye pointi tisa za mechi 13 ndiyo inashika mkia.
  Petrojet iliuanza vizuri mchezo wa jana kufanikiwa kuongoza kwa mabao 2-0 hadi mapumziko, wafungaji Ahmed Raouf dakika ya tatu na Mahmoud Salah dakika ya 10.   Himid Mao jana alicheza kwa dakika zote 90 Petrojet FC ikichapwa 3-2 na Nogoom 

  Lakini kipindi cha pili Petrojet inayofundishwa na kocha mzalendo, Tarek Yehia ikatepeta na kuwaruhusu wanyeji kupata mabao matatu ndani ya dakika saba yaliyofungwa na Ahmed Rabia dakika ya 70, Salah Amin dakika ya 73 na Islam El Far dakika ya 77.
  Nogoom inajiongezea pointi tatu na kupanda hadi nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 12, katika Ligi ambayo Zamalek inaongoza kwa pointi zake 23 za mechi 10, ikifuatiwa na Smouha pointi 19 mechi 12.
  Vigogo wengine wa Misri, Al Ahly wanashika nafasi ya 13 wakiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi sita na Al Masry wapo nafasi ya 15 wakiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi nane.   
  Kikosi cha Nogoom jana kilikuwa; Ahmed Saad, Mahmoud Fathalla, Khaled Abdelrazek/Ahmed Rabia dk61, Micheal Azekhumen, Mahmoud Abdel Halim/Salah Amin dk46, Ahmed Ayman, Islam El Far, Amr El Sisi, Ahmed Sherweda/Ahmed Gamal dk82, Mohamed Hammam na Mohab Yasser.
  Petrojet FC; Mohamed Abou Elnaga, Ahmed El Sebaie, Ibrahim Al Kadi/Ahmed Sobhi dk75, Ahmed Abdel Rasoul, Mohamed Reda, Mahmoud Salah/Ahmed Abdel Rahman Zola dk79, Himid Mao, Mahmoud Emad, Ahmed Raouf/Mohamed Salem dk68, Shimeles Bekele na Mohamed Sanogo ‘Vieira’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIMID MAO ACHEZA MWANZO MWISHO PETROJET YAPIGWA 3-2 UGENINI, ILIONGOZA 2-0 HADI MAPUNZIKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top