• HABARI MPYA

  Wednesday, November 07, 2018

  HENRY MAMBO MAGUMU MONACO, WAPIGWA 4-0 NYUMBANI NA KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA

  KOCHA mpya wa Monaco, Thierry Henry amezidi kuwa katika wakati mgumu baada ya kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Club Bruges kwenye mechi ya Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Kwa matokeo hayo, huku Henry akifikisha mechi tano bila ushindi tangu apewe ukocha wa Monaco, timu hiyo inatolewa kwa sababu haiwezi kufikisha pointi tisa ambazo tayari wanazo Atletico Madrid na Borussia Dortmund.
  Monaco, waliofika Nusu Fainali ya michuano hiyo mwaka 2017, kwa ujumla wamecheza mechi 15 sasa bila ushindi kwenye mashindano yote.


  Thierry Henry (kushoto) akizungumza na beki wake, Djibril Sidibe baada ya mambo kuwa magumu jana 

  Mabao ya Club Bruges jana yalifungwa na Hans Vanaken mawili dakika za 12 na 17 kwa penalti, mshambuliaji Mbrazil, Wesley dakika ya 24 na Nahodha Ruud Vormer dakika ya 85. 
  Henry aliajiriwa mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Leonardo Jardim, lakini hajashinda mchezo wowote kati ya mitano aliyoiongoza timu hiyo hadi sasa ambayo kwenye nafasi za kushuka daraja katika msimamo wa Ligi ya Ufaransa. 
  Henry aliyeshinda Kombe la Dunia na Ufaransa akiwa mchezaji mwaka 1998, hii ni mara ya kwanza anakuwa kocha mkuu baada ya kuwa Msaidizi wa Roberto Martinez timu ya taifa ya Ubelgiji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HENRY MAMBO MAGUMU MONACO, WAPIGWA 4-0 NYUMBANI NA KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top