• HABARI MPYA

  Thursday, November 08, 2018

  CHIRWA AWAACHA MIDOMO WAZI YANGA SC, ASAINI MWAKA MMOJA KUUNGANA NA NGOMA, PLUIJM AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMMBULIAJI wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa amesaini mkataba wa mwaka kujiunga na Azam FC kama mchezaji huru, baada ya kuachana na klabu ya Yanga, pia ya Dar es Salaam.
  Chirwa ametambulishwa leo ofisi kuu za klabu ya Azam FC, Mzizima barabara ya Nyerere mjini Dar es Salaam mbele ya Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’, Meneja Philipo Alando, Ofisa Habari, Jaffar Iddi Maganga na Kocha Mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm. 
  Na baada ya kutambulishwa, Chirwa akasema kwamba amejiunga na Azam FC kukiongezea nguvu kikosi ambacho tayari ni bora ili wafanikishe azam ya kutwaa mataji.
  Kocha Mkuu wa Azam FC, Mholanzi Hans van der Pluijm (kulia) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo, mshambuliaji mpya, Obrey Chirwa 

  Kutoka kulia, Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans van der Pluijm (kulia), mshambuliaji mpya, Obrey Chirwa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin 'Popat' 
  Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin 'Popat' akimkabidhi jezi Obrey Chirwa
  Kutoka kulia, Ofisa Habari, Jaffar Iddi, Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans van der Pluijm), Mtendaji Mkuu Jaffar Abdulrahman 'Popat', mshambuliaji mpya, Obrey Chirwa na Meneja Philipo Alando  

  Mshambuliaji mpya, Obrey Chirwa, akiahidi mambo kishujaa mbele ya Ofisa Habari, Jaffar Iddi

  Kwa upande wake, kocha Pluijm ambaye alifanya kazi na Chirwa katika klabu ya Yanga, alisema kwamba  amefurahi sana kumpata mchezaji huyo anayejituma na mwenye bidii kubwa uwanjani.
  Chirwa sasa anakwenda kukutana na mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aliyewahi kufanya naye kazi FC Platinums ya Zimbabwe na Yanga.
  Kama ilivyokuwa Yanga, Ngoma alianza kuja na baadaye akamvuta Chirwa akimshawishi Pluijm aje kuongeza nguvu na kwa Azam hivyo pia, inaamini Donald amemshawishi tena Pluijm kumsajili mchezaji huyo. 
  Chirwa aliondoka Yanga SC baada ya msimu uliopita, akisema anakwenda Misri ambako pamoja na kuripotiwa alifaulu majaribio, mwishowe amerejea Tanzania na saa anasaini Azam FC.
  Mapema kabla ya kusaini amewahi kuposti picha akiwa na jezi ya Azam FC na ingawa ilipuuzwa na Yanga wakaendelea kujipa matumaini atarejea kwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIRWA AWAACHA MIDOMO WAZI YANGA SC, ASAINI MWAKA MMOJA KUUNGANA NA NGOMA, PLUIJM AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top