• HABARI MPYA

  Saturday, October 13, 2018

  NGASSA ANG’ARA YANGA IKIICHAPA MALINDI FC 2-0 MECHI YA KIRAFIKI KUMUAGA CANNAVARO ZANZIABR LEO

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  YANGA SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar, Malindi FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo.
  Nyota wa mchezo wa leo alikuwa mkongwe, kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa aliyefunga bao moja na kuseti moja katika ushindi huo.
  Ngassa anayecheza Yanga kwa mara ya tatu baada ya kurejea tena msimu huu, alimtilia krosi nzuri Emmanuel Martin kufunga bao la kwanza dakika ya 43 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 60 akimalizia krosi ya Pius Buswita.
  Kocha Msaidizi wa Yanga, Mzambia Noel Mwandila alibadili karibu kikosi chote baada ya bao la pili, lakini matokeo yakagoma kubadilika.    
  Mchezo wa leo ulikuwa maalum kumuaga aliyekuwa Nahodha wake na beki hodari, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyestaafu Mei mwaka huu.
  Nadir alitokea Zanzibar kujiunga na Yanga mwaka 2006 ambako amedumu kwa miaka 12 kabla ya kutungika daluga Mei mwaka huu.
  Kikosi cha Malindi kilikuwa; Ahmed Ali, Omar Yussuf, Muharami Issa, Mohammed Iddi, Ibrahim Abdallah, Ibrahim Novat, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Ali Mkanga, Hajji Chewa, Ali Badru na Mohammed Said.
  Yanga SC; Ramadhani Kabwili, Juma Abdul/Paul Godfrey dk67, Mwinyi Hajji Mngwali, Pato Ngonyani, Cleophas Sospeter/Abdallah Shaibu ‘Ninja’ dk63, Said Juma ‘Makapu’/Raphael Daudi dk67, Mrisho Ngassa, Thabani Kamusoko/Maka Edward dk69, Yussuf Mhilu/Jaffar Abdulrahman dk63, Pius Buswita/Ibrahim AJib dk67 na Emmanuel Martin/Heritier Makambo dk63.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA ANG’ARA YANGA IKIICHAPA MALINDI FC 2-0 MECHI YA KIRAFIKI KUMUAGA CANNAVARO ZANZIABR LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top