• HABARI MPYA

  Saturday, October 13, 2018

  OKWI AFUNGA MAWILI UGANDA YAICHAPA LESOTHO 3-0

  TIMU ya taifa ya Uganda, The Cranes imejiimarisha kileleni mwa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Lesotho jioni ya leo Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, Uganda.
  Kwa ushindi huo, Uganda inafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, ikishinda mbili na kutoa sare, sasa ikifuatiwa na Cape Verde pointi nne za mechi tatu pia, wakati Tanzania yenye pointi mbili sawa na Lesotho ni ya tatu kwa wastani wa mabao.
  Ushindi wa leo wa The Cranes umetokana na mabao ya washambuliaji wake, Emmanuel Okwi  anayechezea klabu ya Simba ya Tanzania aliyefunga mawili dakika za  11 na 63 na Faruku Miya wa Farouk Miya wa HNK Gorica ya Croatia kwa penalti dakika ya 36.

  Emmanuel Okwi (katikati) akishangilia na Faruku Miya (kulia) baada ya wote kufunga leo

  Timu hizo zitarudiana Jumanne Uwanja wa Setsoto mjini Maseru, siku ambayo Cape Verde watakuwa wanarudiana na Tanzania Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam baada ya ushindi wa 3-0 jana nyumbani Uwanja wa Taifa mjini Praia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI AFUNGA MAWILI UGANDA YAICHAPA LESOTHO 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top