• HABARI MPYA

    Sunday, October 28, 2018

    MGOMBEA UENYEKITI WA BODI AAHIDI MAMBO MAZURI SIMBA SC AKICHAGULIWA NOVEMBA 4

    Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
    MGOMBEA Uwenyekiti wa bodi ya klabu ya Simba SC, Swedy Nkwabi amewaomba wanachama wamchague akashirikiane na mwekezaji Mohamed Dewji 'Mo' kuleta maendeleo klabuni.
    Simba ipo kwenye mchakato wa uchaguzi baada ya kumaliza marekebisho ya katika yao, inayowapelekabkatika mfumo mpya wa uwekezaji wa hisa ambao utumiwa na klabu mbalimbali Duniani kwa Sasa.
    Simba wanatarajia kufanya uchaguzi Novemba 4, mwaka huu huku nafasi ya mwenyekiti wa bodi akibaki Nkwabi baada ya Mtemi Ramadhani kujitoa dakika za mwisho. 
    Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye uziduzi wa kampeni zake katika hotel ya Souther Sun, Nkwabi alisema, anaimani kubwa uwezo na sifa anayo ya kuwaeakilisha wanasimba wengi Nchini katika klabu hiyo kwa kushirikiana na Mwekuzaji.

    Swedy Nkwabi amewaomba wanachama wamchague akashirikiane na Mohamed Dewji 'Mo' kuleta maendeleo Simba

    Alisema kuwa endapo atapata nafasi atahakikisha anaondoa makundi ya wanachama ndani ya klabu ya Simba kwa kutengeneza umoja wenye nguvu ndani ya Simba kwa kufuata na kuheshimu katiba.
    "Kwa Sasa mfumo wa uongozi umebadilika, Simba ya Sasa sio ya zamani, inahitaji umakini wa hali ya juu, na kwa kutambua uwezo ninao ndio sababu ya kujitosa kuwania nafasi hii, ili tukaivushe Simba yetu, ni wakati wenu wanasimba kupiga kura ya ndio kwa Swedy ili nikawawakilishe vyema uko katika Bodi,"alisema.
    Aidha Nkwabi anabainisha kwa kuwataka wanasimba kutofanya makosa kwa kuchagua watu kwa mihemko waangalie mtu mwenye sifa kwani huko waendako ni kugumu hivyo wachague watu makini ambao akipata nafasi hiyo ataweza kushirikiana vilivyo.
    Nae Mjumbe wa bodi hiyo Zawadi Kadunda aliyebobea katika masuala ya biashara anawaomba wanasimba kumpa kura za kutosha ili akawatumikie huko.
    "Najitambua uwezo na elimu ninayo ya kuongoza hasa katika Simba ya Sasa, kwani baada ya kubadilishwa kwa mfumo wa uendeshaji ndio maana nikashawishika kugombea ili nilichonacho wanasimba wakipate kupitia uwakilishi wangu huko,"
    Anasema bila ya kuwa na mabadiliko ya kimfumo ndani ya klabu hiyo, asingejitosa kugombea, hivyo kwa kujua umuhimu wa mfumo huu na kutokana na ubobezi alionao akaona ni bora ajitose hivyo anawaomba wanasimba wamchague akawatumikie.
    Nae Mjumbe wa bodi Hussein Kitta anasema alikuwa akiota siku moja Simba iweze kufikia hatua hii, na hivyo imefikia ndio maana kaona aingie akaweke uwezo wake kwa kushirikiana na wengine watakaopata nafasi ili waipeleke Simba mbele zaidi ya Sasa.
    "Mambo ya kufanya Simba ni mengi sana,pamoja na kutoa mchango wangu katika masuala ya mpira, yapo zaidi ya mpira ambayo hata Mimi nina uwezo nayo kwa sababu ya taaluma yangu, kitaalamu Mimi ni mwanasheria ni mhadhiri wa Sheria chuo kikuu Dar es Salaam, cha kwanza kabisa ni kuwaelekeza wanasimba juu ya huu mfumo,"
    Anasema anatambua wanasimba wengi hawautambui vilivyo huo mfumo hivyo atahakikisha eanautambua ili waelewe yatakayofanyika ni kutokana na mfumo na sio vinginevyo.
    Alisema kuwa kule kwenye bodi ndipo mikakati mikubwa inapopangwa sehemu ambapo mwelekeo wa klabu na shughuri zake unatengenezwa kwa hiyo makusudio yake kupitia uzoefu wake ni kusaidiana kuijenga Simba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MGOMBEA UENYEKITI WA BODI AAHIDI MAMBO MAZURI SIMBA SC AKICHAGULIWA NOVEMBA 4 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top