• HABARI MPYA

  Sunday, November 05, 2017

  WYDAD MABINGWA WAPYA WA AFRIKA, WAIPIGA 1-0 AL AHLY

  KLABU ya Wydad Casablanca ya Morocco ndiyo wafalme wapya wa soka barani, baada ya usiku wa jana kuichapa 1-0 Al Ahly ya Misri katika mchezo wa marudiano wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mohammed V mjini Casablanca.

  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee la ushinid, Walid El Karty dakika ya 69 na Wydad wanabeba taji hilo la Afrika kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya kulazimisha sare ya 1-1 mjini Alexandria wiki iliyopita katika fainali ya kwanza.
  Achraf Bencharki, aliyesawazisha bao katika mchezo wa kwanza, ndiye mpishi wa bao la jana la El Karty kutokana na kutia krosi nzuri. 
  Ushindi huo unamaanisha Wydad wanabeba taji hilo kwa ya kwanza baada ya miaka 25 tangu walipolitwaa mara ya kwanza mwaka 1992 kwa kuifunga Al Hilal ya Sudan kwenye fainali, wakati huo bado michuano hiyo inaitwa Klabu Bingwa Afrika.
  Jina la michuano hiyo lilibadilishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwaka 1997 wakati mfumo mpya wa mashindano na zawadi ulipoanza kutumika.
  Kwa ushindi huo, Wydad inapatiwa zawadi ya dola za Kimarekani Milioni 2.5 na uhakika wa kujipatia dola Milioni 1 nyingine kwa sababu kwa kuwa bingwa wa Afrika, itacheza michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA Desemba mwaka huu Falme za Kiarabu (UAE). 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WYDAD MABINGWA WAPYA WA AFRIKA, WAIPIGA 1-0 AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top