• HABARI MPYA

  Sunday, November 05, 2017

  SIMBA SC IKIIPIGA MBEYA CITY LEO INARUDI KILELENI

  Na David Nyika, MBEYA
  SIMBA SC inaweza kurudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo iwapo itawafunga wenyeji, Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine mjini hapa. 
  Azam FC ilipanda kileleni mwa Ligi Kuu jana baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, bao pekee la kinda Yahya Zayed dakika ya 90.
  Ushindi huo umeifanya timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi tisa, ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga walio nafasi ya pili pamoja na Mtibwa Sugar.
  Simba SC ina pointi 16 baada ya kucheza mechi nane na leo inaingia katika mchezo wa kwanza kati ya miwili mfululizo ya Mbeya, mwingine dhidi ya Tanzania Prisons Novemba 18, ikisaka lazima ushindi kurudi kileleni.
  Kocha wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog ataendelea kuwakosa wachezaji wake watatu majeruhi wa muda mrefu, kipa Said Mohammed ‘Nduda’ na mabeki Shomary Kapombe na Salim Mbonde, lakini hana wasiwasi atashinda leo.
  Omog alionekana ni mwenye kujiamini wakati anawaongoza vijana wake mazoezini kwenye Uwanja wa Sokoine asubuhi.
  Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi anataka kuondoa imani kwamba yeye anaweza kufunga Dar es Salaam pekee kwa kuhakikisha anafunga leo Sokoine.
  Upande wa Mbeya City, kocha Mrundi, Nsanzurwimo Ramadhani amesema hawaihofii Simba SC kwa sababu ni timu ambayo wapo nayo kwenye Ligi Kuu.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC IKIIPIGA MBEYA CITY LEO INARUDI KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top