• HABARI MPYA

  Monday, November 06, 2017

  POLE KOCHA LWANDAMINA…APATA MSIBA ZAMBIA, ANAONDOKA LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mzambia wa Yanga, George Lwandamina anatarajiwa kuondoka leo usiku kurejea kwao Zambia kufuatia kufiwa na mpwa wake. 
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam, Lwandamina amesema kwamba amepata msiba nyumbani na analazimika kuondoka mara moja.
  Lwandamima amesema kwamba anatarajia kurejea nchini Jumanne wiki ijayo kuendelea na maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kocha wa Yanga, George Lwandamina amefiwa na mpwa wake Zambia 

  Jumamosi Yanga ililazimishwa sare ya ya 0-0 na wenyeji, Singida United Uwanja wa Namfua mkoani Singida katika mchezo wa Ligi Kuu.
  Sare hiyo ya pili mfululizo baada ya Jumamosi iliyopita pia kutoka 1-1 na mahasimu wao wa jadi, Simba inaifanya Yanga ifikishe pointi 17 baada ya kucheza mechi tisa, wakati Singida inafikisha pointi 14 baada ya mechi tisa pia.
  Mabingwa hao watetezi, watateremka tena uwanjani Novemba 19 kumenyana na Mbeya City Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. 
  Pole kocha Lwandamina. Na Mungu ampumzishe kwa amani mpendwa wetu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLE KOCHA LWANDAMINA…APATA MSIBA ZAMBIA, ANAONDOKA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top