• HABARI MPYA

    Friday, November 03, 2017

    MWASHIUYA, MARTIN NA MLIPILI WATEULIWA KIKOSI CHA OLIMPIKI

    Na Rehem Lucas, DAR ES SALAAM
    WINGA wa Yanga, Geoffrey Bahati Mwashiuya ni kati ya wachezaji 35 walioteuliwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 kwa ajili ya mechi za kufuzu Olimpiki ya mwaka 2020 Jijini Tokyo, Japan. 
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala, Jijini Dar es Salaam wakati wa kutaja kikosi hicho, Kocha Msaidizi wa timu za vijana Tanzania, Oscar Milambo amesema wachezaji hao watapunguzwa hadi kubaki 25.
    Milambo aliyefanya shughuli hiyo kwa niaba ya bosi wake, Mdenmark, Kim Poulsen amesema kwamba kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 6, mwaka huu katika hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume.
    Geoffrey Mwashiuya ni kati ya wachezaji 35 walioteuliwa kwenye kikosi cha awali cha U- 23  

    Milambo amesema wachezaji wote walioteuliwa wana umri usiozidi miaka 20, kwa sababu wameteua vijana ambao hata timu ikifuzu Olimpiki ya Tokyo 2020 wataweza kucheza michuano hiyo kwa kuwa ndiyo watakuwa wamefikisha miaka 23 ambayo ndio kikomo.
    Kikosi kamili cha U-23 kinaundwa na makipa; Metacha Mnata (Azam FC), Joseph Ilunda (JKT Ruvu) na Liza Mafwea (Tanzania Prisons).
    Mabeki ni Paulo Lyungu (Maji Maji), Yussuf Mlipili (Simba), Abbas Kapombe (Ndanda mkopo kutoka Azam), Salum Chukwu (Singida United), Cleotas Sospeter (Yanga), Idrissa Mohammed (Maji Maji), Bakari Kijuji (Tanzania Prisons), Joseph Prosper (Azam FC), Masoud Abdallah ‘Cabaye’ (Azam FC), William John (Ruvu Shooting) na Yusuph Anthony (Yanga).
    Viungo ni Adam Salamba (Stand United), Omary Mponda (Ndanda FC), Eliud Ambokile (Mbeya City), Geoffrey Mwashiuya (Yanga), Emmanuel Kakuti (Mbeya City), Emmanuel Martin (Yanga), Medson Mwakatunde (Mbeya City) na Derueshi Shaliboko.
    Washambuliaji ni Ismail Aidan (Mtibwa Sugar), Salum Kihimbwi (Mtibwa Sugar), Hassan Mganga ((Mtibwa Sugar), Awad Salum (Njombe Mji FC), Awesu Ally (Mwadui FC), Yahya Zayed (Azam FC),Ayoub Masoud (Ndanda FC), Baraka Majogoro (Ndanda FC), Mohammed Habib (Miembeni FC), Agathon Mapunda (Njombe Mji), Faisal Salum Abdallah (JKU) na Yusuph Kagoma (Singida United).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWASHIUYA, MARTIN NA MLIPILI WATEULIWA KIKOSI CHA OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top