• HABARI MPYA

    Tuesday, November 07, 2017

    MTIBWA SUGAR YAREJEA MANUNGU KUJIPANGA NA KAGERA BAADA YA ‘KUZINYANYASA’ TIMU ZA LINDI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    BAADA ya ushindi wa mechi mbili mfululizo za kirafiki mkoani Lindi, Mtibwa Sugar inarejea Turiani mkoani Morogoro kuanza maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mtibwa watakuwa wenyeji wa ndugu zao, Kagera Sugar ya Bukoba katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Novemba 18, Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
    Na Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur amesema kwamba kikosi kililala Dar es Salaam jana kikitokea na Lindi na leo mchana kinaunganisha safari ya kurejea Turiani kwa basi lao walilopewa hivi karibuni na wamiliki, Superdoll. 
    Henry Joseph (kushoto) amefunga mabao matatu katika mechi mbili za Mtibwa Sugar dhidi ya Monaco na Black Mob mjini Lindi

    Ikiwa Lindi, Mtibwa Sugar inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Zuberi Katwila ilicheza mechi mbili za kirafiki, Jumapili ikishinda 5-0 dhidi yas Monaco na jana ikashinda 3-1 dhidi ya Black Mob.
    Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Henry Joseph Shindika alifunga katika mechi zote mbili, dhidi ya Monaco akifunga mabao mawili na dhidi ya Black Mob bao moja.
    Kevin Sabato Kongwe naye akafunga kwenye mechi hizo, dhidi ya Monaco bao moja na mawili dhidi ya Black Mob, wakati mabao mengine yalifungwa na Riffat Khamisi na Saleh Hamisi katika mchezo wa kwanza, mechi zote zikichezwa Uwanja wa Ilulu.
    Mabingwa hao wa Ligi Kuu 1999 na 2000, walikwenda Lindi wakitoka Mtwara ambako Jumamosi walilazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Ndanda FC katika mchezo wa mwingine wa Ligi Kuu.
    Swabur amesema kwamba timu itaendelea kuwakosa awachezaji watatu, kipa Shaaban Kado, beki Salum Kanoni na mshambuliaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAREJEA MANUNGU KUJIPANGA NA KAGERA BAADA YA ‘KUZINYANYASA’ TIMU ZA LINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top