• HABARI MPYA

    Thursday, November 02, 2017

    MAJI MAJI WAPO NYUMBANI WAKIIKARIBISHA STAND UNITED KESHO LGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kwa mchezo mmoja kufanyika kesho Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, ambako mwenyeji Maji Maji FC wataikaribisha Stand United ya Shinyanga.
    Ligi Kuu itaendelea tena Jumamosi kwa michezo mingine mitano kuchezwa kwenye viwanja tofauti, kama wa kesho na hiyo itaanza Saa 10:00 jioni.
    Michezo hiyo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Singida United itakayocheza na Yanga SC kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida wakati Tanzania Prisons itakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba  mjini Bukoba, Kagera.
    Wachezaji tegemeo wa Maji Maji, Danny Mrwanda na Jerry Tegete (kushoto)
    Njombe Mji kwa upande wake watakuwa wenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe huku Mtibwa Sugar ikisafiri kutoka Morogoro kwenda Mtwara kucheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Hizo ni mechi zitakazochezwa saa 10.00 jioni.
    Mchezo pekee utakaofanyika saa 1.00 usiku utakuwa ni kati ya Azam FC na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam.
    Jumapili kutakuwa na michezo miwili ya Ligi Kuu ambako Lipuli ya Iringa itakuwa mwenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Samora wakati Simba itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi hizo zitaanza saa 10.00 jioni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAJI MAJI WAPO NYUMBANI WAKIIKARIBISHA STAND UNITED KESHO LGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top