• HABARI MPYA

  Sunday, November 19, 2017

  LWANDAMINA: ITAKUWA MECHI NGUMU, LAKINI TUTAPIGANA TUSHINDE

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amesema kwamba mechi dhidi ya Mbeya City leo itakuwa ngumu, lakini watapambana washinde ili wasiachwe mbali sana na mahasimu wao, Simba katika mbio za ubingwa.
  Yanga wanaikaribisha Mbeys City jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Na baada ya Simba kushinda 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons jana Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya imefikisha pointi 22 na kujitanua kileleni mwa Ligi Kuu.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Lwandamina amesema kwamba wanaingia kwenye mchezo mgumu, lakini watapigana washinde. “Mbeya ni timu nzuri na kwa sababu imefungwa mechi mbili mfululizo leo watakuwa wakali sana, lakini tutajitahidi tushinde,”amesema Mzambia huyo.
  George Lwandamina (kulia) akiwa na Msaidizi wake, Nsajigwa Shadrack (kushoto) 
  Yanga hawawezi kurudi kileleni hata wakishinda leo, lakini wanachoweza ni kujisogeza karibu na mahasimu wao hao wa jadi iwapo wataifunga Mbeya City.
  Azam FC inahitaji kushinda 13 -0 dhidi ya wenyeji Njombe Mji FC Uwanja wa Saba Saba ili kupanda kileleni, vinginevyo kwa ushindi wowote watawafikia tu kwa pointi Simba, lakini kwa kuzidiwa wastani wa mabao watabaki nafasi ya pili. 
  Mechi nyingie ya kukamilisha mzunguko wa 10 leo itapigwa Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wakiwakaribisha ndugu zao, Kagera Sugar.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA: ITAKUWA MECHI NGUMU, LAKINI TUTAPIGANA TUSHINDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top