• HABARI MPYA

  Saturday, November 04, 2017

  AZAM FC YAPAA KILELENI LIGI KWA BAO LA DAKIKA YA MWISHO CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imekaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Ahsante kwake mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 90, kinda Yahya Zayed na sasa Azam FC inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi tisa, ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga walio nafasi ya pili pamoja na Mtibwa Sugar.

  Mfungaji wa bao pekee la Azam FC leo Uwanja wa Azam Complex, Yahya Zayed

  Simba SC inaweza kurudi kileleni iwapo itaifunga Mbeya City kesho katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Idd Kipagwile/Joseph Mahundi dk63, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Waziri Junior dk81, Mbaraka Yusuph/Peter Paul dk70, Enock Atta Agyei na Yahya Zayd.
  Ruvu Shooting: Bidii Hussein, George Amani, Mau Bofu, Frank Msese, Shaibu Nayopa, Zuberi Dabi, Baraka Mtuwi, Shaaban Msala, Issa Kanduru/Said Dilunga dk83, Ishala Juma/Jamal Soud dk49 na Abdulrahman Mussa.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPAA KILELENI LIGI KWA BAO LA DAKIKA YA MWISHO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top