• HABARI MPYA

  Tuesday, March 21, 2017

  YANGA YAPELEKWA ALGERIA KUWANIA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itamenyana na Mouloudia Club d'Alger, maarufu kama MC Alger ya Algeria katika mchujo wa kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya droo iliyopangwa mchana huu mjini Cairo, Misri yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
  Droo hiyo imehusisha timu zilizovuka hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho dhidi ya zilizotolewa kwenye hatua hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Timu zilizotolewa Ligi ya Mabingwa zitamenyana na zilizosonga mbele Kombe la Shirikisho katika mechi za nyumbani na ugenini kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani.
  Mechi za kwanza zinatarajiwa kucheza wikiendi ya Aprili 7 hadi 9 na marudiano yanatarajiwa kuwa wikiendi ya Aprili 14 hadi 16, mwaka huu.
  Yanga SC imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanacio Jumamosi Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia.
  Matokeo hayo yanamaanisha Yanga inatolewa kwa mabao ya ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAPELEKWA ALGERIA KUWANIA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top