• HABARI MPYA

  Monday, March 20, 2017

  SIMBA SC KUMENYANA NA MERERANI STARS LEO

  Na Clement Shari, ARUSHA 
  VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC leo wanatarajiwa kuwa na mchezo wa kirafiki na Mererani Stars utakaofanyika Uwanja wa CCM Mererani, Arusha.
  Mchezo huo unakuja siku moja baada ya Wekundu hao wa Msimbazi, kuitoa Madini FC ya Arusha katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi wa 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha jana.
  Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo dakika ya 55 kwa kichwa baada ya kuufikia mpira wa juu uliomshinda beki wa Madini, Hamisi Hamisi na sasa Simba inakwenda Nusu Fainali.
  Beki wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala'  anatarajiwa kucheza dhidi ya Mererani Stars leo
  Katika mchezo wa leo Mererani, viingilio vinatarajiwa kuwa Sh. 3,000 kwa wakubwa na Sh. 1,000 kwa watoto.
  Msemaji wa Mererani Stars, Japhary Matimbo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba maandalizi yako vizuri na wanatarajiwa kutoa ushindani kwa vigogo hao wa soka ya Tanzania.
  Wakati huo huo: JKT Oljoro leo wanajitupa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa kumenyana na Cosmo Politan ya Dar es Salaam katika mchezo wa mchujo wa kuwania kucheza Ligi Daraja la  Kwanza msimu ujao.
  Kocha wa JKT Oljoro, Emanuel Masawe ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba  
  maandalizi yote kuelekea pambano hilo yamekamilika na wanachohitaji wao ni  
  ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kureje Daraja la Kwanza msimu ujao.
  Tayari Oljoro imekwishacheza mechi mbili na kushinda moja na kutoka  
  sare moja. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUMENYANA NA MERERANI STARS LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top