• HABARI MPYA

  Sunday, March 05, 2017

  SAMATTA MOTO CHINI, APIGA MBILI ZOTE GENK YAUA 2-1 UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MCHEZAJI ‘Almasi’ kutoka Jamhuri ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amefunga mabao yote mawili, KRC Genk Genk ikishinda 2-1 dhidi ya Club Brugge Uwanja wa Luminus Arena katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
  Samatta ambaye kwa sasa ndiye mshambuliaji tegemeo wa Genk, alifunga mabao hayo dakika za tano na 42 na mara zote akimalizia pasi za kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero, huku bao la wageni likifungwa na Mcolombia Jose Heriberto Izquierdo dakika ya 43 kwa pasi ya Myahudi, Lior Refaelov. 
  Mbwana Samatta akipongezwa na wenzake jana baada ya kufunga mabao mawili

  Mbwana Samatta shughulini katika mchezo wa jana Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk

  Samatta jana amefikisha mabao 14 katika mechi 46 alizoichezea Genk tangu asajiliwe Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC.
  Kati ya mechi hizo 45, 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 28 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 27 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 17 msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na tisa msimu huu na katika mabao hayo 14, nane amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Ryan, Castagne, Brabec, Colley, Uronen, Berge, Malinovskyi, Pozuelo, Boetius/Heynen dk80, Writers na Samatta/Naranjo dk84.
  Club Brugge: Butelle, Van Rhijn, Simons/Rotariu dk82, English, Refaelov/Wesley dk61, Foxes/Diaby dk61, Izquierdo, Vanaken, Denswil, Creator na De Bock.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA MOTO CHINI, APIGA MBILI ZOTE GENK YAUA 2-1 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top