• HABARI MPYA

  Wednesday, March 22, 2017

  BOCCO APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu ya goti la mguu wa kulia.
  Bocco aliumia Januari 28, mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba, siku ambayo alifunga bao pekee timu yake ikishinda 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi alisema kwamba Bocco yuko Afrika Kusini akifanyiwa matibabu ya goti hilo.
  “Alianza kufanyiwa matibabu hapa nyumbani baada ya kuumia, lakini bahati mbaya imekuwa inachukua muda kupona, hivyo uongozi umeona mchezaji huyo akatibiwe huko,”alisema.
  John Bocco ‘Adebayor’ yupo Afrika Kusini kwa matibabu ya goti la mguu wa kulia

  Jaffar alisema mbali na Bocco, wachezaji wengine majeruhi Azam, beki Aggrey Morris na kiungo Mcameroon, Stephanie Kingue wataendelea na matibabu Dar es Salaam baada ya timu hiyo kurejea kutoka Swaziland walikofungwa 3-0 na wenyeji Mbabane Swallows Jumapili na kutolewa katika hatua ya 32 ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Kipigo cha 3-0 mwishoni mwa wiki kinafanya Azam FC itolewe kwa jumla ya mabao 3-1, baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top