• HABARI MPYA

  Monday, March 20, 2017

  BLAGNON AREJEA NA MABAO SIMBA SC, AWAFUNGA 1-0 MERERANI STARS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi baada ya jioni ya leo kuifunga 1-0 Mererani Stars katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa CCM Mererani, Arusha.
  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo, pekee Muivory Coast, Frederick Blagnon mapema kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Hijja Ugando.
  Katika mchezo huo, kocha Mcameroon Joseph Marius Omog alianzisha wachezaji wengi ambao hakuwatumia kwenye mchezo wa jana dhidi ya Madini FC Simba ikishinda 1-0 Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, bao pekee la Mrundi, Laudit Mavugo dakika ya 55.
  Muivory Coast, Frederick Blagnon amerejea na mabao Simba SC ikiilaza 1-0 Mererani Stars leo

  Blagnon alikuwa anacheza kwa mara ya kwanza Simba SC leo tangu arejee kutoka Oman wiki iliyopita, ambako alikwenda kwa mipango ya kujiunga na Oman Club kwa mkopo, iliyoshindikana baada ya Waarabu kuchelewa kuomba Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC). 
  Blagnon alijiunga na Simba SC Julai mwaka jana kutoka African Sports ya kwao Ivory Coast, lakini Desemba mwaka jana klabu hiyo ikaridhia kumtoa kwa mkopo Uarabuni kabla ya mpango kushindikana na kurejea.
  Kikosi cha Simba kilikuwa; Peter Manyika, Hamad Juma, Mohammed Mussa, Novaty Lufunga, Vincent Costa, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Hijja Ugando, Mwinyi Kazimoto, Juma Luizio/Jamal Mnyate, Frederick Blagnon/James Kisandu na Pastory Athanas.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BLAGNON AREJEA NA MABAO SIMBA SC, AWAFUNGA 1-0 MERERANI STARS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top