• HABARI MPYA

  Sunday, November 06, 2016

  PLUIJM AFUMUA KIKOSI, KAKOLANYA ANAANZA

  Na Mwandishi Wetu,  MBEYA
  KIPA mpya wa Yanga kutoka Prisons, Benno Kakolanya leo atadaka kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Amissi Joselyn Tambwe ataanzia benchi Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amefanya mabadiliko makubwa kutoka kikosi kilichlambwa 2-1 na Mbeya City katikati ya wiki, leo akiwaanzisha pamoja washambuliaji wa zamani wa FC Platinums ya Zimbabwe, Mzambia Obrey Chirwa na Mzimbabwe Donald Ngoma.
  Benno Kakolanya leo atadaka kwa mara ya kwanza Yanga ikimenyana na timu yake ya zamani, Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya

  Na ajabu zaidi leo ni kwamba, Pluijm amemuanzisha kinda Yussuf Mhilu wakati Juma Mahadhi na kipa aliyesimama langoni dhidi ya Mbeya City akitunguliwa mabao mawili ya mashuti ya mbali, Deo Munishi 'Dida' hata benchi hawapo. Hassan Kessy ameanzishiwa benchi na beki ya kulia leo ameanza Mbuyu Twite na langoni yupo Benno Kakolanya.
  Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Benno Kakolanya, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Thabani Kamusoko, Yussuf Mhilu, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Deus Kaseke.
  Katike benchi wapo Ally Mustafa 'Barthez', Oscar Joshua, Matheo Anthony, Hassan Kessy, Vincent Andrew, Amissi Tambwe na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AFUMUA KIKOSI, KAKOLANYA ANAANZA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top