• HABARI MPYA

  Wednesday, October 19, 2016

  BABU NGASSA AZUIWA KUKAA BENCHI LA TOTO MECHI NA YANGA LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa zamani wa Simba, Khalfan Ngassa ameziwa kukaa kwenye benchi la Toto Africans ya Mwanza kama kocha msaidizi kwa sababu hana vyeti.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema kwamba baba huyo wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa amekuwa akiketi kwenye benchi la Toto kwa mechi tatu mfululizo zilizopita za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
  Taaifa hiyo imesema kwamba Babu Ngassa aliongoza timu hiyo kwenye mchezo Na. 62 dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 7, 2016; mchezo Na. 67 dhidi ya Mbao FC uliofanyika Oktoba 12, 2016 na Mchezo Na. 79 dhidi ya Majimaji ya Songea uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu.
  Khalfan Ngassa (kulia) ameziwa kukaa kwenye benchi la Toto Africans kuanzia leo mechi na Yanga 

  Lakini TFF imjesema kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 72 (3) (5) ya Ligi Kuu, Kocha Mkuu anatakiwa kuwa na Leseni ya chini kuanzia Daraja B ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) na Daraja C kwa Kocha Msaidizi pia kutoka CAF.
  Na kutokana na Idara ya Ufundi ya TFF kuthibitisha kuwa Ngassa hana leseni yoyote ya ukocha - hastahili kukaa kwenye benchi la timu ya Toto Africans kama kocha mkuu au kocha msaidizi.
  "Kitendo kinachofanywa na Toto Africans ni ukikwaji wa kanuni na ni vema uongozi wa Toto ukamwondoa Khalfan Ngassa kwenye benchi ili kuepuka adhabu. Kipendele cha (7) cha kanuni hiyo ya 72, inaelekeza adhabu kuwa inaweza kutozwa si chini ya Sh 500,000 (shilingi laki tano),"imesema taarifa hiyo.
  TFF pia imezikumbusha klabu nyingine zote kuwa kuanzia msimu ujao wa 2017/18 wa Ligi Kuu ya Vodacom, kocha anayestahili kukaa kwenye benchi ni yule mwenye leseni Daraja A kwa nafasi ya Kocha Mkuu na angalau Leseni Daraja B kwa kocha msaidizi.
  Zuio hilo linakuja saa chache tu kabla ya Toto kuivaa Yanga SC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza jioni ya leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BABU NGASSA AZUIWA KUKAA BENCHI LA TOTO MECHI NA YANGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top