• HABARI MPYA

  Sunday, February 07, 2016

  YANGA SC YAZINDUKA, YAITANDIKA 4-0 JKT RUVU, MSUVA APIGA MBILI TAIFA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara bila ushindi ikifungwa na Coastal Union 2-0 Tanga na kutoa sare ya 2-2 na Prisons mjini Mbeya, Yanga SC leo imezinduka.
  Mabingwa hao watetezi leo wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ushindi huo, uliotokana na mabao ya Simon Msuva, Issofou Boubacar na Donald Ngoma unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 43 baada ya kucheza mechi 18, ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi 42 sawa na Azam FC.

  Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Simon Msuva aliifungia Yanga SC bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali la umbali wa mita 27 baada ya kupokea pasi ya beki wa kulia Juma Abdul. 
  Winga wa kimataifa wa Niger, Issoufou Boubacar aliifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 44 baada ya kupokea pasi ya Msuva na kipindi cha pili, mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma akaifungia timu hiyo bao la tatu dakika ya 63.
  Msuva akahitimisha sherehe za mabao za Yanga SC kwa kufunga la nne dakika ya 90 na ushei akimalizia pasi ya Deus Kaseke, ambaye naye alipewa pasi na Paul Nonga.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma/Godfrey Mwashiuya, Malimi Busungu/Paul Nonga dk46 na Issoufou Boubacar/Deus Kaseke dk54.
  JKT Ruvu; Shaaban Dihile, Michael Aidan, Paul Mhidze, Nurdin Mohammed, Ramadhani Madenge, Nashon Naftali, Mussa Juma, Hassan Dilunga, Gaudence Mwaikimba, Samuel Kamuntu na Emmanuel Pius/Amos Mgisa dk77.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAZINDUKA, YAITANDIKA 4-0 JKT RUVU, MSUVA APIGA MBILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top