• HABARI MPYA

    Monday, February 22, 2016

    SIMBA SC, YANGA NA AZAM VITA YAHAMIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

    RATIBA 16 BORA KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION
    Februari 24, 2016
    Yangs SC Vs JKT Mlale (Saa 10:30 jioni U/Taifa)
    Februari 26, 2016
    Ndanda FC Vs JKT Ruvu (Saa 10:00 jioni U/Nagwanda
    Coastal Union Vs Mtibwa Sugar (Saa 10:00 jioni U/Mkwakwani)
    Februari 27, 2016
    Mwadui FC Vs Rhino Rangers (Saa 10:30 jioni U/Mwadui)
    Prisons Vs Mbeya City (Saa 10:30 jioni U/Sokoine)
    Februari 28, 2016
    Simba SC Vs Singida United (Saa 10:00 jioni U/Taifa)
    Panone FC Vs Azam FC (Saa 10:00 jioni U/Ushirika)
    Toto Africans Vs Geita Gold (Saa 10:30 jioni U/ Kirumba)
    Simba SC watamenyana na Singida United Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    MICHUANO ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuendelea wiki hii mzunguko wa nne katika hatua ya 16 bora, kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
    Jumatano Februari 24, 2016 kutakua na mchezo mmoja tu, ambapo timu ya Young Africans watawakaribisha maafande wa JKT Mlale kutoka mkoani Ruvuma katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10:30 jioni.
    Michezo miwili itachezwa siku ya Ijumaa ambapo, Ndanda FC watakua wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
    Jumamosi Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo.
    Mzunguko huo wa nne utakamilika siku ya Jumapili ambapo, Simba SC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
    Bingwa wa Kombe hilo, ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara bingwa wake akicheza Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC, YANGA NA AZAM VITA YAHAMIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top