• HABARI MPYA

  Sunday, February 07, 2016

  HAJIB AING’ARISHA SIMBA SC SHINYANGA, YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KAMBARAGE

  Na Princess Asia, SHINYANGA
  BAO pekee la mshambuliaji Ibrahim Hajib limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage, Shinyanga leo.
  Ushindi huo unaifanya Simba SC iendelee kukaa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, ikifikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 18. 
  Hajib alifunga bao hilo dakika ya 45 baada ya kupata pasi ya kisigino ya Mganda, Hamisi Kiiza ingawa sifa zimuendee Mwinyi Kazimoto aliyepika bao hilo.
  Ibrahim Hajib akishangilia baada ya kufunga leo Uwanja wa Kambarage

  Hajib angeweza kuondoka na mabao mawili leo Uwanja wa Kambarage, kama si mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na kipa Andrew Ntalla wa Kagera dakika a 83.
  Refa Mathew Akrama wa Mwanza alimtoa nje kwa kadi nyekundu Daudi Jumanne wa Kagera Sugar dakika ya 91 kwa lugha chafu.
  Kocha wa Kagera Mohammed ‘Adolph’ Rishard alikuwa akiwalalamikia marefa tangu mchezo unaendelea na baada ya mechi, wachezaji wa timu hiyo waliwavamia waamuzi, kabla ya kuondolewa na Polisi.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Juuko Murshid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamisi Kiiza/Brian Majwega dk67, Ibrahim Hajib na Hajji Ugando/Danny Lyanga dk56.
  Kagera Sugar; Andrew Ntalla, Salum Kanoni, Juma Jabu, Job Ibrahim, Shaaban Ibrahim, George Kavilla, Adam Kingwande, Daudi Jumanne, Martin Lupert, Mbaraka Yussuf, Paul Ngalyoma. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAJIB AING’ARISHA SIMBA SC SHINYANGA, YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top