• HABARI MPYA

    Thursday, February 25, 2016

    LIGI DARAJA PILI YAFIKIA TAMATI, NANI KUPANDA LA KWANZA?

    LIGI Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL) inatarajiwa kufikia tamati wikiendi hii kwa michezo 12 ya makundi yote, A, B, B, C na D kuchezwa kwenye viwanja toafuti nchini, huku kila kundi likitoa timu moja ya juu kupanda Daraja la Kwanza.
    Kesho Ijumaa, michezo mitatu ya kundi C itachezwa katika raundi hiyo ya mwisho, Villa Squad watacheza dhidi ya Mshikamano (Mabatini, Mlandizi), Abajalo Dar v Karikaoo FC (Karume) na Changanyikeni watakuwa wenyeji wa Cosmopolitan katika uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.
    Abajalo watamenyana na Kariakoo Lindi kesho Uwanja wa Karume
    Kundi A, Jumamosi Green Warriors watawakaribisha Abajaro Tabora katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Transit Camp watakua wenyeji wa Mvuvumwa uwanja wa Kambarage Shinyanga, huku siku ya Alhamis Singida United watacheza dhidi ya Mirambo uwanja wa Namfua mjini Singida.
    Jumamosi Kundi C, Alliance Schools watakua wneyeji wa Bulyankulu katika uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya  Pamba FC uwanja wa Karume Musoma, na Madini FC watakua wenyeji wa AFC Arusha uwanja wa Mbulu.
    Kundi D, Jumapili Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Wenda FC uwanja wa CCM Mkamba, Sabasaba watakua wenyeji wa The Mighty Elephant uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku Mbeya Warriors wakicheza dhidi ya African Wanderes katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
    Timu moja ya kwanza kutoka katika kila kundi itapanda moja kwa moja ligi daraja la kwanza (StarTimes League) msimu ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI DARAJA PILI YAFIKIA TAMATI, NANI KUPANDA LA KWANZA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top