• HABARI MPYA

  Sunday, February 07, 2016

  SAMATTA ACHEZA MECHI YA KWANZA GENK IKISHINDA 1-0 LIGI KUU UBELGIJI

  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Samatta jana amecheza mechi yake ya kwanza katika klabu yake mpya, KRC Genk ya Ubelgiji ikishinda 1-0 ugenini, bao pekee la Thomas Buffel dakika ya 63 dhidi ya Mouscron-Peruwelz katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.
  Samatta aliyesajiliwa diridha dogo mwezi ulkiopita kutoka TP Mazembe ya DRC, aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.
  Mbwana Samatta jezi namba 77 akiichezea Genk kwa mara ya kwanza jana

  na pamoja na kucheza kwa dakika 17 tu katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, maarufu kama Pro League, Samatta aliwatia misukosuko mabeki wa Mouscron-Peruwelz. 
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Bizot, Walsh, Dewaest, Kabasele, Hamalainen, Ndidi, Kumordzi/Malinovsky dk58, Buffel, Bailey, Kebano/Buyens dk83 na Karelis/Samatta)
  Dk73.
  Samatta aliwatia misukosuko mabeki wa Mouscron-Peruwelz
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ACHEZA MECHI YA KWANZA GENK IKISHINDA 1-0 LIGI KUU UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top