• HABARI MPYA

  Sunday, February 07, 2016

  NGASSA ATOA PASI YA BAO LAKINI FREE STATE YAPIGWA 5-2 NA MAMELODI AFRIKA KUSINI

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa ametoa pasi ya bao timu yake, Free State Stars ikifungwa mabao 5-2 na Mamelodi Sundowns katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini leo Uwanja wa James Motlatsi. 
  Ngassa aliyekosa mechi mbili zilizopita kutokana na kuwa majeruhi, alimlamba chenga Hlompho Kekana kabla ya kumpasia Danny Venter aliyefunga dakika ya kwanza tu. Bao lingine la Free State limefungwa na Mashego dakika ya 90.
  Mabao ya Mamelodi yamefungwa na Wayne Arendse, Keagan Dolly, Leonardo Castro, Khama Billiat na Mogakolodi Ngele.
  Mrisho Ngassa (kushoto) ametoa pasi ya bao leo Free State ikifungwa 5-2 na Mamelodi

  Arendse alifunga dakika ya 41, Dolly dakika ya 57, Castro dakika ya 61, Billiat dakika ya 75 na Ngele dakika ya 87.
  Kikosi cha Free State Stars kilikuwa; Diakite, Mashego, Sankara/Gopane dk72, Nkausu/T. Shabalala dk55, Tlhone, Venter, Masehe, Chabalala, Ngasa, Ngcobo/Somaeb dk57 na Mohomi.
  Mamelodi Sundowns: Sandilands, S. Zwane/Mashaba dk54, Mbekile, Langerman, Nthethe, Arendse, Kekana, Modise, Dolly, Billiat/Ngele dk79, Castro/Soumahoro dk75.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA ATOA PASI YA BAO LAKINI FREE STATE YAPIGWA 5-2 NA MAMELODI AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top